amreezle

amreezle

Sunday, April 29, 2012

Shambulizi la gruneti lauwa Nairobi!!

Posted  on April 30, 2012 

Polisi nchini Kenya wanasema shambulizi la guruneti kwenye Kanisa moja jijini Nairobi limeuwa mtu mmoja Jumapili na kuwajeruhi vibaya wengine zaidi ya 10. Mpaka sasa hakuna aliyedai kufanya shambulizi hilo katika Kanisa hilo linalojulikana kama God’s House of Miracle International church lililoko katika mji mkuu wa Kenya.
Kwa mujibu wa VOA Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika siku 6 baada ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya kuonya juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi mjini Nairobi. Ubalozi huo ulitoa ujumbe huo ukionya raia wa Marekani kutahadhari.
Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na majengo mashuhuri ya serikali mjini Nairobi yakashambuliwa na magaidi. Aidha taarifa hiyo ya ubalozi ilisema wakati mahsusi wa shambulizi hilo hujulikani lakini yaaminika wanaopanga shambulizi hilo wamo katika hatua za mwisho.

JK KUBWAGA MAWAZIRI WENGI WA ZAMANI,SURA MPYA ZATABIRIWA

Posted on April 30, 2012 

Wakati mawaziri wanaounda Serikali ya Awamu ya Nne wakiendelea kupata usingizi wa mang’amung’amu kwa hofu ya kupanguliwa, kuna taarifa kwamba idadi kubwa ya mawaziri wa zamani wataachwa na sura mpya hususan vijana kutawala baraza jipya.
Kwa mujibu wa Mwananchi joto la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri limeshika kasi baada ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam juzi na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa chama hicho, kuwataka mawaziri wanaoandamwa na kashfa mbalimbali katika wizara zao, kuachia ngazi.
Taarifa ya Rais Kikwete kutaka kusuka upya Baraza la Mawaziri ilitangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizikia kwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CCM.
Vyanzo vya Mwananchi vimeeleza kuwa mbali na Rais kutumia kigezo cha udhaifu uliobainishwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), atawaengua pia wale wanaoshindwa kuwajibika na wale wenye kasi ndogo ya uongozi. Kusoma zaidi bofya Read more »

Semina ya Uamsho Columbus, OH

Tunawakaribisha wote kwenye Semina ya Uamsho itakayofanyika hapa Columbus, Ohio wiki ijayo kuanzia tarehe 4-6 Mei. Semina itaendeshwa na Mch. Douglas Mmari kutoka Minnesota. Kutakuwa na waimbaji maarufu wakiongozwa na Dada Flora Mbasha kutoka Tanzania na Printze Ngosso wa hapa Columbus. Kwa maelezo zaidi ingia kwenye hii link.

Saturday, April 28, 2012

The town of Bagamoyo ni TANZANI!!


HISTORY OF BAGAMOYO TOWN

The town of Bagamoyo, Tanzania, was founded at the end of the 18th century. It was (also spelled Bagamojo) the original capital of German East Africa and was one of the most important trading ports along the East African coast. Today the town has about 30,000 inhabitants and is the capital of the District of Bagamoyo, recently being considered as a world heritage site.
The second church built by the missioners in Bagamoyo


Bagamoyo was the most important trading entrepot of the east central coast of Africa in the late 19th century. Bagamoyo's history has been influenced by Indian and Arab traders, by the German colonial government and by Christian missionaries.

About 5 km south of Bagamoyo, the Kaole Ruins with remnants of two mosques and a couple of tombs can be dated back to the 13th century, showing the importance of Islam in those early Bagamoyo times.

Kaole Ruins in Bagamoyo, Tanzania

Until the middle of the 18th century, Bagamoyo was a small and insignificant trading center where most of the population were fishermen and farmers. The main trading goods were fish, salt, and gum, among other things.
The Old Church at Bagamoyo, Tanzania
 In the late 18th century Muslim families settled in Bagamoyo, all of which were relatives of Shamvi la Magimba in Oman. They made their living by enforcing taxes on the native population and by trading in salt, gathered from the Nunge coast north of Bagamoyo. In the first half of the 19th century, Bagamoyo became a trading port for ivory and the slave trade, with traders coming from the African interior, from places as far as Morogoro, Lake Tanganyika and Usambara on their way to Zanzibar. This explains the meaning of the word Bagamoyo ("Bwaga-Moyo") which means "Lay down your Heart" in Swahili. It is disputed whether this refers to the slave trade which passed through the town (i.e. "give up all hope") or to the porters who rested in Bagamoyo after carrying 35 lb cargos on their shoulders from the Great Lakes region (i.e. "take the load off and rest"). Since there is little evidence to support that Bagamoyo was a major slave port (Kilwa, much further south, has earned this status), and that tens of thousands of porters arrived at Bagamoyo annually in the latter half of the 19th century, it is more likely that the name of the town derives from the latter interpretation.


The slave trade in East Africa was officially prohibited in the year 1873, but continued surreptitiously well to the end of the 19th century.


In 1868, Bagamoyo local rulers, known as majumbe, presented the Catholic "Fathers of the Holy Ghost" with land for a mission north of the town, the first mission in East Africa. This caused resistance by the native Zaramo people which was mediated by representatives of Sultan Majid and, after 1870, by Sultan Barghash. Originally the mission was intended to house children who were rescued from slavery, but it soon expanded to a church, a school, and some workshops and farming projects.
But Bagamoyo was not only a trade centre for ivory and copra; it was also a starting point for renowned European explorers. From Bagamoyo they moved out to find the source of the River Nile and explored the African inner lakes. Some of these were Richard Francis Burton, John Hanning Speke, Henry Morton Stanley and James Augustus Grant. Although often believed so, David Livingstone had never been to Bagamoyo in his lifetime.

Only after his death he was laid out in the Old Church's tower (nowadays named Livingston Tower) to wait for the high tide to come in and ship his body to Zanzibar.
Bagamoyo was the German headquarters of German East Africa (first under the auspices of the German East African Company and then the German Imperial Government) between 1886-1891. Dar es Salaam became the new capital of the colony in 1891. The town was apparently the (1895) birth place of SS-Oberführer Julian Scherner. During World War I, in 1916, a British air attack and naval bombardment was launched on Bagamoyo, the Germans were overrun and the German garrison taken.
When the German Empire decided to build a railway from Dar es Salaam into the interior in 1905, Bagamoyo's importance began to decline.

JK aitisha Kamati Kuu CCM ghafla

Posted on April 28, 2012

Wakati joto la wabunge, vyama vya siasa na wanaharakati nchini kutaka mawaziri waliohusishwa na kashfa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wajiuzuluzu likizidi kupanda, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha ghafla cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya siasa nchini.
Habari zilizolifikia gazeti la Mwananchi na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, zilieleza kuwa kikao hicho kitafanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Ingawa Nape alisema hawezi kutaja ajenda za kikao hicho kwa kuwa ni siri, habari kutoka baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, zilidokeza kuwa hakuna namna, Rais Kikwete akakwepa kuzungumzia shinikizo la mawaziri hao kujiuzulu.Kusoma zaidi bofya Read more »
Posted on April 28, 2012 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amewajibu jeshi la polisi mkoani Mwanza kuwa, anawakaribisha wote wanaotangaza kutaka kumkamata kufuatia madai ya kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Mwananchi kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, kutangaza kumchukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu huyo.
Akiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Sahara, Dk Slaa alitoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuwakamata wale wote waliohusika na vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.Kusoma zaidi bofya Read more »

Thursday, April 26, 2012

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA KWENYE SHEREHE ZA MUUNGANO.

Postd on April 27, 2012 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa uhuru jijini Daresalaam kuongoza maadhimisho ya miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar alhamisi asubuhi.
Rais Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere katika uwanja wa Uhuru jijini Daresalaam
(Picha wa hisani ya Michuzi)

HALAIKI YA WANAFUNZI YAPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA

Posted on April 27, 2012 

Hawa si wanafunzi wa jamhuri ya kikomunisti ya China bali ni wanafunzi wa Tanzania wakifanya vitu wakati wa sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye uwanja wa uhuru Daressalaam Tanzania.
Halaiki ya wanafunzi wapatao 1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani waliipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika alhamisi katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao, ni wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kauli mbiu ni “Shiriki kikamilifu katika Sensa na mchakato wa Mabadiliko ya Katiba”.Kwa hisani ya full shangwe.

WAPINZANI WA SIMBA WAMEWASILI DAR

Posted on  April 27, 2012
Wakati msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Al Ahly Shandy ya Sudan ukiwasili nchini leo kwa ajili ya kukwaana na Simba, mgeni rasmi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Timu hizo zitakwaana Aprili 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).
Akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, kocha mkuu wa Al Ahly Kouk Mohammed aliiambia mamapipiro blog kwamba mchezo huo uantarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani Simba ni timu nzuri.
Alisema anaifahamu Simba kama moja ya timu mahiri barani Afrika sambamba na kuwa na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa hali ambayo itawafanya wawe makini zaidi pindi watakaposhuka dimbani.
Hata hivyo kocha huyo raia wa Tunisia alisema kwamba huenda wakaathiri kidogo na hali ya hewa ya Tanzania kutokana na kuwa tofauti na Sudan ingawa watajitahidi kukabiliana nayo.
Kikosi cha Al Ahly kinaundwa na wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo wawili kutoka Nigeria , mmoja kutoka Mali na mwingine kutoka Mali huku wachezaji wawili wakiichezea timu ya Taifa ya Sudan .
Al Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku Simba ikibebwa na bao la ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya kwenda kufungwa 3-1.
Katika hatua nyingine tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika vituo tofauti jijini Dar es salaam huku waamuzi wa mchezo huo kutoka Swaziland Nhleko Simanga Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze Mbongiseni Elliot na Kamishna wa Kayijuga Gaspard wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili leo.
Katika kujiandaa na mchezo huo, Simba imepiga kambi eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambapo kocha mkuu wa Simba Mserbia Milovan Cirkovic amejinasibu kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo katika jiji la Shandy , Sudan .
Chanzo: www.Bongostaz.blogspot.com

WAZIRI MAIGE ASEMA ALILIPA DOLA 410,000 LEMBELI APINGA, ASEMA ALIINUNUA KWA DOLA 700,000 TASLIMU

Posted on April 27, 2012

SIKU chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).Kusoma zaidi bofya Read more »

Waziri akiri kununua nyumba ya mamilioni

Posted on April 26, 2012 
Waziri wa maliasili na utalii Tanzania Ezekiel Maige.
Siku chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).
Awali, habari zilizolifikia gazeti la Mwananhgi zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate. Kusoma zaidi bofya Read more »

SIKU LINAH ALIPOWAPA RAHA WATU WA COLUMBUS OHIO

Posted  on April 26
Linah akifanya vitu vyake katika ukumbi wa Monkey’s Bar Columbus Ohio.Jumamosi hii April 28 atazazamua New York New York.
Linah na Aj jukwaani.
Linah akipewa love na mashabiki wa Ohio.
Wapenzi wa Linah Ohio wakiselebuka.
Bi.Janita wa pili kulia kwa raha zake akiselebuka na mashabiki wengine wa Lina jijini Ohio. Kwa picha zaidi bofya Read more »

Wednesday, April 25, 2012

Amran

Kibaki asema serikali haitakubali kujitenga kwa jimbo la Pwani

Posted on April 25, 2012 by amran

Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imetoa onyo kwa makundi yanayopigania kujitenga kwa jimbo la pwani kutoka taifa la Kenya akihutubia kikao cha bunge mjini Nairobi kwa mara ya kwanza tangu kuidhinishwa katiba mpya rais Mwai Kibaki amesema serikali haitakubali kujitenga kwa jimbo la Pwani kutoka taifa la Kenya.
Kwa mujibu wa VOA rais huyo amesema jimbo la Pwani ni ardhi ya Kenya na jimbo hilo halitakubaliwa kujitenga. amesema Kenya ni taifa moja juhudi zozote za kulihgawanya taifa hilo zitakataliwa.Kusoma zaidi bofya Read more »

Lipumba: JK amemziba Pinda mdomo

Posted on April 25, 2012 by amran
Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka jamii kutomhukumu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kushindwa kushughulikia madai ya wabunge kutaka mawaziri wajiuzulu akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete amemziba mdomo.
Kwa mujibu wa Mwananchi akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema hata kama Pinda angekuwa na utashi wa kuzungumzia suala hilo, asingeweza kusema chochote kwa kuwa Rais Kikwete alimziba mdomo… “na suala hilo pia liko juu yake.” Kusoma zaidi bofya Read more »

Mzee atuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12!

Posted on April 25, 2012 by amran
Huku tukiendelea kupambana na ufisadi jamii yetu bado ina kazi kubwa kwa masuala mengine kama vile ubakaji ungana na Habari leo wakiripoti balaa hili.
Polisi katika Mkoa wa Kusini, inatarajia kumfikisha katika Mahakama ya Mwera Wilaya ya Kati Unguja, mkazi wa kijiji cha Machui, Suleiman Khamis Mihayo (67) kujibu mashitaka ya kumbaka msichana wa miaka 12 (jina tunalihifadhi) katika eneo la Machuwi Wilaya ya Kati Unguja.
Mkuu wa Dawati la Watoto katika kituo cha Polisi cha Mwera, ACP Khadija Haji Khatib alisema Mihayo aliripotiwa wiki iliyopita baada ya mtoto huyo kutuhumiwa kuiba mali za Mihayo ambazo ni nguo pamoja na nazi.
Hata hivyo, mtoto huyo baada ya kuhojiwa na polisi, inadaiwa alimtuhumu Muhayo kufanya mapenzi naye kwa muda mrefu bila ya kumpa malipo ya fedha ndio maana akachukua mali hizo kujilipa ujira wake.Kusoma zaidi bofya Read more »

Hakimu ambembeleza Lulu mahakamani

Posted on April 24, 2012 
Mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu akilia wakati alipofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Picha na Michael Jamson.
Msanii wa filamu, Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akibubujikwa machozi kiasi cha kumfanya Hakimu Ritha Tarimo ambembeleze ili kumnyamazisha. Lulu anashtakiwa mahakamani hapo kwa kutuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba na alifikishwa jana kwa mara ya pili akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza na Polisi.
Kwa mujibu wa mwananchi Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi akiwa katika basi dogo la Magereza pamoja na mahabusu wengine wanawake ambalo lilikuwa likisindikizwa na magari mengine mawili na alikuwa chini ya ulinzi wa askari sita wa kike wa Magereza na askari mmoja wa kike wa Polisi wakishirikiana na askari wa kiume wa Magereza zaidi ya sita. Kusoma zaidi bofya Read more »

Pinda aziba masikio mawaziri kujiuzulu -Ufisadi Maliasili unatisha

Posted in Uncategorized on April 24, 2012 by sunday Shomari
Wakati wabunge wakiendelea kusaini fomu ya majina ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni jana alikwepa kuzungumzia hatua za kinidhamu dhidi ya mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mwananchi akiahirisha Mkutano wa Saba bungeni Dodoma, Pinda hakugusia suala la kujiuzulu kwa mawaziri wanane na badala yake alisema: “Siku zote Serikali imekuwa tayari kupokea ushauri wa Bunge baada ya kusikiliza mjadala na mapendekezo ya waheshimiwa wabunge.’’
Baada ya kuahirishwa kwa Bunge hadi Juni 12, mwaka huu. Pinda akiwa nje ya Bunge alikwepa kuzungumzia suala hilo licha ya kubanwa na waandishi wa habari na badala yake alicheka: “Haahaa,” kisha akaingia kwenye gari na kuondoka. Kusoma zaidi bofya Read more »

Tuesday, April 24, 2012

SAKATA YA MAWAZIRI TANZANIA SASA WALIPUANA

Posted on April 23, 2012 
Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu ametuhumu Naibu wake Athuman Mfutakamba akisema ndiye mhusika mkuu wa tuhuma za ufisadi zilizoelekezwa kwake kiasi cha wabunge kufikia hatua ya kumshinikiza ajiuzulu.
Kwa mujibu wa Mwananchi mbali ya mawaziri hao, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu ametoa waraka unaombebesha mzigo Waziri wake, Dk Cyril Chami akisema alimpa ushauri wa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege kupisha uchunguzi, lakini hakutekeleza. Kusoma zaidi bofya Read more »

Monday, April 23, 2012

Operesheni Uwajibikaji bungeni.

Postd on April 23, 2012
Mjumbe wa NEC CCM ndugu Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Musoma Vijijini amesaini waraka wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Serikali. Amekuwa Mbunge wa 74 kufanya hivyo na Mbunge wa 6 kutoka CCM. #OperesheniUwajibikaji-Zitto Kabwe-Fb.

PLOTS FOR SALE LOW DENSITY IN TANZANIA

Plots for sale at the following locations:
Mapinga Bagamoyo Road, 40m by 20m most plots 200 meters off Dar-Bagamoyo Rd.
Price-Tshs. 15 mill. approximately.
Also Njiro Hill Arusha near Tanzania Nuclear Regulatory Authority head office. Price Tshs 90 mill.

LINAH -LIVE IN BOSTON MASS..SAT MAY 12 “TAMANI USA TOUR” INAWASHA MOTO BALAAAAAAAA!!

Posted on April 23, 2012 

Je Pinda kumfuata Lowassa?

Posted on April 23, 2012

TIMU YA WATANZANIA DMV IMEKAMILISHA LENGO LAKE LA KUINGIA LIGI YA DIASPORA WOLD CUP 2012

Posted on April 23, 2012 
Na Ebou Shatry
Tanzania DMV imekamilisha madhumini na malengo ya kujiandaa rasmi na ligi ya Diaspora World Cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland, mwanzoni mwa mwenzi huu wa Mei chini ya mdhamini wa timu hiyo Abdallah wa Vizion One.
Taarifa kwa wachezaji wote mnaombwa kuzingatia muda wa mazoezi mliopangiwa ili kuwa makini na malengo yaliokusudiwa ya ligi ya Diaspora World cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland,
Pia katika bahati hii ya kushiriki kwenye ligi ya Diaspora World Cup, na kufanikisha malengo yaliokusudiwa, timu hiyo ya TZ DMV inawaomba Watanzania wote ushirikiano wenu wa kila hali ili kuipa changamoto timu ya Watanzania DMV pamoja na wachezaji, katika burudani inayopendwa na wengi ulimwenguni, karibuni karibuni sana siku ya sherehe za ufunguzi April 28th ndani ya Discovery Stadium uliopo Germantown SoccerPlex. Stadium.
Milango inatunguliwa saa sita mchana ambapo jamii zote zitawasili kuunga mkono time zao zilizoingia katika ligi hiyo kitaifa kama Diaspora World Cup pamoja na ngoma za kiasili, nyote mnakaribishwa.
Vile vile vigogo wengi wamethibitisha uwepo wao ikiwa ni pamoja na HE Eklil Hakimi, Mheshimiwa Balozi wa Afghanistan katika Umoja wa Mataifa, HE Joseph Foe-Atangana, Mheshimiwa Balozi wa Cameroon katika Umoja wa Mataifa, HE Perezi K. Kamunanwire, Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Marekani, HE Adebowale mimi. Adefuye, Mheshimiwa Balozi wa Nigeria nchini Marekani, HE Devinda R. Subasinghe, aliyekuwa Balozi wa Sri Lanka, Waziri Johnny Moloto, Mkuu wa Mission wa Afrika Kusini nchini Marekani, Jenerali Emmanuel Maganga, wa Tanzania katika Ubalozi wa Marekani, na kamanda Luther Reynolds, Mkuu wa Polisi wa Germantown atakuwepo,
Adress MD. 14501 Schaeffer Rd
Germantown, MD20874

Watu kadhaa watiwa mbaroni Zanzibar

Posted on April 23, 2012

Jeshi la polisi Zanzibar limewatia mbaroni watu zaidi ya 12 kwa madai ya kukataa kutii amri ya jeshi hilo ya kutakiwa kuondoka katika viwanja vya baraza la wawakilishi, walipokwenda kuonana na Spika na Baraza hilo Pandu Ameir Kificho.

CHANZO:Mzalendo.net

Stock Market Newsletter

Posted on April 22, 2012
David Magness
JAPAN has now SHUT DOWN 53 of its 54 Nuclear Reactors…since the Fukushima Daiichi Reactor was damaged by a Tsunami and Earthquake March 11, 2011…and has returned to fossil fuels…and all building of nuclear reactors has stopped in Japan…
…This is causing the Japanese economic recovery to SLOW DOWN…and will cause parts of Southeast Asia to be affected…
…At the moment…ONLY CHINA is building Nuclear reactors…at a rate of one per week…These are small reactors…used for communities of 20,000 residents or less…The COMMUNIST PARTY is afraid of a CIVIL WAR by the 80% “HAVE NOTS”…who have been neglected by THE PARTY for the past 60 years…since CHINA became “RED”… in OCTOBER 1949…
…Many of these communities still don’t have electric light…so the SAFETY of the new reactors IS IN QUESTION…as the Communist Party rushes to CATCH UP…
…Technically…the market LAST WEEK Avoided a “SELL SIGNAL” by ONLY days…USING the old TURTLE TRADING SIGNAL…that says IF after a MARKET TOP…IF the market CLOSES below the LOW of the PAST 20 days…the MARKET RALLY would BE OVER…
…IT DIDN’T…so this newsletter comes to you ONE WEEK LATE…with the “RALLY INTACT”…but STILL waiting for this to “Play Out”…
…SUMMARY…Using W.D. GANN’s formula…we have a SERIOUS MARKET DATE coming up…May 15th…IF we get past THIS DATE…the NEXT BUMPER will be JUNE 11-15th…At that POINT…we believe the Springtime Rally will FINALLY be over UNTIL FALL…Until…OCTOBER…ONE MONTH BEFORE the Elections…
…TSP Participants should MOVE to the C FUND…[S&P 500]…

Sarkozy ashindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi

Posted on April 22, 2012

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist, Francois Hollande amepata ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Ufaransa Jumapili, akijipatia asili mia 29.3 za kura. Mpinzani wake kiongozi wa vyama vya kihafidhina rais Nicplas Sarkozy amepata asili mia 26 za kura.
Kwa mujibun wa VOA wanasiasa hao wawili watapambana katika duru ya pili hapo Mei 6. Matokeo hayo yalitarajiwa kutokana na uchunguzi kadha wa maoni uliofanywa kabla ya uchaguzi wa Jumapili ukionyesha kwamba Hollande atamshinda Sarkozy katika duru ya kwanza na ya pili. Kusoma zaidi bofya Read more »

Ridhiwani Kikwete amshukia Millya

Posted on April 22, 2012 

Baada ya kujiengua UVCCCM Mwenyekiti wa Umoja huo mkoani Arusha amepokea dozi ya vijembe kutoka viongozi mbali mbali wa Umoja huo pamoja na CCM.
Ungana na Nipashe upate yale aliyotoa Ridhwani Kikwete kwa kiongozi huyo wa zamani wa UVCCM
Mtoto wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha, James Ole Millya.
Millya alijiengua kutoka CCM na kujiunga CHADEMA kutokana na kile alichoeleza kuwa chama tawala kimekuwa mfano wa gari lililosheni pancha, hivyo halifai kwa safari.
Hata hivyo, baada ya Millya kuondoka CCM, taarifa zilizopatikana mkoani humo zilieleza kwamba aliondoka akiwa na takribani Shilingi milioni 2, mali ya UVCCM.
Taarifa hizo ndizo zimemuibua Ridhiwani akichangia katika mtandao wa kijamii wa Tunuru la Afrika na kusema Millya asubiri utaratibu unafuata. Kusoma zaidi bofya Read more »

BANDARI YA DAR YAIBUA MAPYA-Wabunge wahoji iweje serikali itegemee upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni

Posted 0n April 22, 2012 Ujenzi wa gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam Jumamosi ulizua tafrani bungeni kutokana na mabishano makali baina ya Kamati ya Miundombinu inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na baadhi ya wabunge.
Mabishano hayo yalitokea kuhusu upembuzi yakinifu unaodaiwa kufanywa na kampuni ya kigeni China Communication Construon Company (CCC), kuhusu ujenzi wa gati hizo na kuweka ghalama ya dola za Marekani milioni 325.
Wabunge wengi walihoji iweje serikali itegemee upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni ambayo wakati huo huo ndiyo inatarajiwa kupewa zabuni ya kujenga gati hizo.
Mbunge wa Ubungo, Chadema John Mnyika, alitaka serikali iteue kampuni inayojitegemea kwa ajili yaa kufanya upya upembuzi yakinifu ili kujua gharama halisi zitakazotumika kujenga gati hizo.
Alisema kutegemea upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni kunaweza kulitia hasara kubwa taifa hivyo alitahadharisha serikali ijiridhishe kwanza kabla ya kutoa zabuni ya ujenzi.
Awali, katika ripoti ya Kamati ya Miundombinu, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Peter Serukamba, ilisema Mamlaka ya Bandari TPA ikishirikiana na kampuni hiyo ya China, ilishafanya upembuzi yakinifu hivyo hakuna haja ya kurudia upya.
Serukamba alisema kuanza upya kufanya upembuzi yakinifu ni kupoteza muda wa ujenzi wa gati hizo ambazo zilianza kuzungumzwa tangu mwaka 2008.

Thursday, April 19, 2012

KITENDAWILI CHA UFISADI TANZANIA BADO NGUMU – Ufisadi wa mabilioni kila kona

Posted on April 20, 2012

Ufisadi , ufisadi , ufisadi uwajibikaji utakuja lini hii ni wazi kama nilivyosema awali kazi ya mapambano 5Tanzania bado ni kubwa! fuatana na gazeti la Mwananchi kwa ripoti ifuatayo Wabunge Jumanne waliijia juu Serikali kwa matumizi mabaya ya fedha za umma na ufisadi ulijitokeza kwenye taasisi zake mbalimbali katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, mwaka jana.
Hasira za wabunge hao zilitokana na ripoti tatu za Kamati za Bunge; Mashirika ya Umma (POAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Serikali Kuu (PAC) kuonyesha upotevu wa mabilioni ya shilingi yaliyotumika katika nyanja mbalimbali ikiwemo mishahara hewa na mikataba mibovu.
Mbunge wa Longido (CCM), Michael Laizer alisema ni aibu kila mwaka kuwa na ripoti za wizi wa mali za umma lakini Serikali inakaa kimya. Kusoma zaidi bofya Read more »

KIBAO CHA LEO KUTOKA KENYA -SIRI YA PENZI

Posted on April 20, 2012 

Kimbunga cha Ole Millya chazidi kuifagia CCM

Posted in Uncategorized on April 20, 2012 by sunday Shomari

Kasi ya wanachama wa CCM kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema mkoani Arusha imezidi kuongezeka baada ya wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wilayani Ngorongoro kukihama chama hicho jana.
Kwa mujibu wa Mwananchi mbali na viongozi hao, pia Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga na Diwani wa Kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema, mkoani Mwanza Hamis Mwagoa, jana walitangaza kuhamia Chadema.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema atachukua rasmi kadi ya Chadema kesho akiwa na wenzake kadhaa ambao hakutaka kuwataja.Kusoma zaidi bofya Read more »

NIMR IMEGUNFUA KIFAA KIPYA CHA KUPIMA KIFUA KIKUU

Posted on April 20, 2012 
Dr.-Mwele-Ntuli-Malecela.
Taasisi ya taifa ya utafiti ya magonjwa ya binadamu (NIMR) imegundua kifaa kipya kijulikanacho kama Genexpert kwa ajili kupima ugonjwa wa kifua kikuu(TB)
Akizungumza katika mkutano wa 26 wa taasisi ya tafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR)mratibu wa tafiti za kifua kikuu katika kituo cha NIMR Mbeya Dkt.Elias Nyanda alisema kuwa kifaa hicho kimethibitishwa na shirika la afya ulimwenguni(WHO).
Alisema kuwa kifaa hicho cha kisasa kina gundua vimelea vya kifua kikuu vyenye vina saba ambavyo vinagundua wadudu walioko kwenye ugonjwa wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili na mgonjwa akapata majibu yake.
Aidha alisema kuwa faida ya kifaa hiki cha kisasa ni pamoja na kugundua kifua kikuu na usugu wa dawa ambapo kifaa kilichokuwa kinatumika awali cha darubini hakikuwa na uwezo huo.
Faida nyingine ni kupunguza uwezo wa kuambukiza ugonjwa huo ambapo hapo awali wagonjwa wa kifua kikuu walioonekana kuwa na ugonjwa huo lakini baada ya kupimwa wakaonekana hawana kwa asilimia 60.
“Kifaa hiki kinagundua kwa haraka sana usugu mwingi ambao mgonjwa amekaa nao kwani mtu akiachwa bila kutibiwa ni wazi kuwa atasambaza mapema kwa watu wengine”alisema Nyanda.
Hata hivyo alitaja changamoto zinazowakabili kutokana na kifaa hicho kuwa ni pamoja na gharama kubwa sana lakini watengenezaji na mashirika ya kifedha wanaja
ribu kupunguza bei kwa nchi zinazoendelea ili kila nchi iweze kuwa na kifaa hicho.
Mbali na hayo alisema kuwa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa mkoa unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa asilimia nyingi wa wagonjwa ndiko wanapotokea.
CHANZO:FULLSHANGWE

SPIKA WA BUNGE TANZANIA AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI

Posted on April 20, 2012

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pomoja na katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kumaliza mazungumzo naye Ofisini kwake Dodoma alhamisi. Balozi Sefua alimtembelea Spika wa Bunge Ofisi kwake mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Sudan na Sudan kusini zaonywa juu ya kurudi vitani

Posted on April 19, 2012

Mkuu wa Umoja wa mataifa amesema Sudan Kusini kulikalia kimabavu eneo la uzalishaji mafuta la Heglig ni kinyume cha sheria na kukiuka utaifa wa nchi jirani ya Sudan.
Kwa mujibu wa VOA akiongea na waandishi wa habari mjini New York alhamisi katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliwaomba Sudan Kusini kuondoa majeshi yao kwenye eneo hilo la mpakani lenye utajiri wa mafuta ambalo linadaiwa na nchi zote mbili.
Bw.Ban pia aliitaka Sudan kuacha kufanya mashambulizi na kupiga mabomu maeneo ya Sudan Kusini na kuondoka kutoka kwenye eneo lenye mzozo la Abyei.

Makada CCM wamfuata James Millya Chadema

Posted on April 19, 2012 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Arusha kimezidi kutikisika baada ya viongozi wake kuendelea kujiondoa na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Siku mbili, baada ya Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James Ole Milya, kujiunga na Chadema, Diwani wa CCM, kata ya Sombetini mkoani humo, Alfonce Mawazo, naye amejiondoa na kujiunga na Chadema. Kusoma zaidi bofya Read more »

Zitto azilipua bungeni Tanesco, ATCL

Posted  on April 19, 2012 

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imependekeza kwa serikali iwakamate na kuwafikisha mahakamani maofisa wa serikali walioingia mkataba wa ukodishaji wa ndege ya ATCL, Air Bus 420-214, mwaka 2007.
Hali kadhalika, kamati hiyo imelishutumu Shirika la Umeme nchini (Tenesco), kwa kufanya manunuzi ya Sh. bilioni 600 bila kufuata sheria za manunuzi.
Kwa mujibu wa Nipashe hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, wakati akiwasilisha taarifa yake, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2010.Kusoma zaidi bofya Read more »

DR.MAGUFULI AUGUA GHAFLA NA KULAZWA YUKO ICU

Posted on April 19, 2012 by Amran

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa habari leo taarifa za kuugua kwa Waziri huyo zilitangazwa jana bungeni na Naibu Spika, Job Ndugai, wakati akiahirisha kikao cha Bunge mchana.
Ndugai alisema awali Magufuli alipelekwa hospitalini hapo akisumbuliwa na shinikizo la damu.
“Baada ya kufika hospitalini na kupatiwa matibabu alibainika kusumbuliwa na kichomi upande wa kushoto… bado amelazwa hospitalini na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikwenda kumwangalia,” alisema.
Pia Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amenusurika kifo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, kupata ajali Morogoro. Kwa mujibu wa Ndugai, ajali hiyo ilitokea jumanne saa 12.15 asubuhi baada ya gari lake kugongwa na lori na kupinduka. Kusoma zaidi bofya Read more »

HONGERA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI

Posted on April 19, 2012 by Amran
Wabunge wapya wa Afrika Mashariki wakipongezana kushoto Makongoro Nyerere na mpiganaji Shyrose Bhanji.(Picha na Mohamed Mambo).

DIDIER DROGBA AFANYA VITU VYAKE

Posted  on April 19, 2012 by AMRAN

Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba akishangilia bao lake pekee alilofunga dakika ya pili ya dakika za majeruhi baada ya kutimu dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London, England usiku huu katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya mabingwa watetezi, Barcelona ya Hispania. Chelsea sasa inahitaji sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano ugenini, Uwanja wa Camop Nou ili kutinga fainali, ambako itacheza na mshindi kati ya Bayern Munich ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania. Mechi ya kwanza jana mjini Munich, Real walifungwa 2-1 na wanahitaji ushindi japo wa 1-0 nyumbani, Santiago Bernabeu ili kutinga Fainali.

Kanye West to Big Sean: 'I Want You to Be Better Than Me'


In an interview with Power 106, Big Sean discussed his next album and revealed advice given to him by Kanye West. Sean mentioned that as his mentor, Yeezy wants him to be better than himself and Jay-Z. "Kanye said 'I want you to be better than me and better than [Jay-Z],' he shared. 'I want you to be the best because you’re the younger generation. We’re passing our secrets on to you. If you don’t take this to new heights and new levels, then what the fuck are we doing this for?’ That’s the...Read Full Story

Kanye West Wants Big Sean To Be Bigger Than Jay-Z? Errr Sure All He Needs To Do Is Eat More! April 19, 2012

Big Sean has recorded a massive success with the album he released from the stables of G.O.O.D Music. “Finally Famous” has sold lots of copies worldwide and label mate Kanye wants Big Sean to be better than he and Jay-z. Big Sean in an interview with Power 106 disclosed Kanye’s position on his success. According to Kanye : I want you to be the best because you’re the younger generation. We’re passing our secrets on to you. If you don’t take this to new heights and new levels, then what...Read Full Story

Obama Calls Kanye West a “Jackass” Again on April 19, 2012

Beware,  Kim Kardashian: President Barack Obama  still has mixed feelings about  Kanye West. Back in September 2009, Obama, 50, famously let his opinion be known about West’s onstage ambush of  Taylor Swift  at the MTV Video Music Awards, calling the rapper, 34, a “jackass” for the stunt. In a brand-new interview in the May issue of The Atlantic ,  the President explains that he prefers the music of  Beyonce ‘s husband  Jay-Z  over Jay’s collaborator and friendly rival West. “Although I...Read Full Story

LOL At Theraflu’s Response To Kanye West Changing ‘Theraflu’ Single Title..


Doooooon do it! Theraflu’s parent company has got bars.. Kanye recently changed the name of his disso track ‘Theraflu” after allegedly feeling the heat from the company. The single cover which also featured a picture of the popular drug was also changed to a plain white bottle. Novartis recently issued a statement to TMZ denying forcing the mega producer to change the title… “Novartis Consumer Health did not ask that the name be changed — that request would be way too cold...Read Full Story

Kanye West’s “Theraflu” Becomes “Way Too Cold,” Gets NSFW Album Artwork

on April 19, 2012  
Kanye West as changed the name of his latest song "Theraflu" which created much controversy upon its release earlier this month. The rapper is now calling the song "Way Too Cold" and changing the cover art to a bottle of milk. West named the song after the cold medicine from big pharmacy firm Novartis. The company issued a statement later on, "We in no way endorse or approve of the references or use of the image and likeness of Theraflu in this manner." It was not explained in his Twitter...Read Full Story

Kanye And Future In Studio


( 4UMF NEWS ) Kanye And Future In Studio: Kanye West is definitely cooking up something G.O.O.D.! He has been holed up in the lab lately with a slew of artists. Check out Yeezy with Future: Related articles Kanye Dumps Kim? (4umf.com) Kanye Changes Theraflu Song Title (4umf.com) Hip-Hop Rumors: Kanye West Denies Calling Kim Kardashian His “Beyonce” (allhiphop.com)Read Full Story

Kanye West Wants To Make it Clear That He Never Said Kim Kardashian was his Beyonce

on April 19, 2012 
Kanye West  has made it really clear the he did not say that   Kim Kardashian  was his  Beyonce . A comment began circulating in which Kanye compared Kim to Beyonce. Even SNL spoofed the rapper’s supposed words! He said: “…of course there are a lot of media inaccuracies surrounding this past couple of weeks, especially the ‘She’s my Beyonce’ quote. I would never compare anyone to my friend’s wife…Come on now, that doesn’t even sound like me, If I don’t say something in a rap or on...Read Full Story

Wednesday, April 18, 2012

SHUKRAN ZA RAIS WA JUMUIYA YA WATANZANIA

Posted in Uncategorized on April 19, 2012 

Nachukua fursa hii kuwashukuru rasmi kwa uchaguzi wa April 15 ambao umetupatia uongozi katika Jumuiya yetu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka mitano. Kwa hakika ushindi si kwa viongozi waliochaguliwa isipokuwa ni ushindi kwa Jumuiya yenyewe. Tulipo leo sio tulipokuwa April 14. Kwa pamoja tumeonyesha nia ya kuunganisha nguvu zetu rasmi na kuleta umoja ambao utasaidia katika maslahi yetu wote kijamii pamoja na taifa letu tunalolipenda– Tanzania.
Sisi mliotuchagua kuongoza juhudi hizo tuna jukumu la kuhakikisha tunatetea, kusikiliza na kuendeleza haki na maslahi ya kila mtanzania. Moyo tulioonyesha katika uchaguzi huu uendelee kuwa chachu ya kuhakikisha tunafanya kazi kwa pamoja, kuinua Jumuiya yetu mpaka pale ambapo tunadhani inastahili kuwepo.
Kama tulikwaruzana katika mchakato huu basi tusameheane, tusirudie makosa na tuangalie mbele kama Jumuiya yenye umoja, upendo na ustahimilivu.
Maana halisi ya Demokrasia iliyokomaa ni kwamba baada ya uchaguzi kwisha Kazi na kipindi muhimu cha kufanya kazi kwa pamoja kinaanza.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Jumuiya DMV
Wenu ,
Rais,
Iddi Sandaly.

KWAHERI DISCOVERY

Posted in Uncategorized on April 19, 2012 
Hii ndio taswira ya chombo cha anga cha Marekani Discovery kama ilivyochukuliwa juu ya jengo la VOA Washington Dc. Kama inavyoonekana ikipelekwa kwenye nyumba yake ya kupumzishwa kwani haitatumika tena huko Chantilly Virginia.

SIMBA YAZIDI KUKARIBIA UBINGWA BARA

Posted in Uncategorized on April 19, 2012 

Mchezaji Uhuru Selemani wa timu ya Simba ya Tanzania kushoto akishangilia goli la kwanza alilofunga dhidi ya timu ya JKT Ruvu pamoja na na wachezaji wenzake Gervas Kago kulia na Patrick Mafisango, Simba imecheza na JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Simba imeshinda magoli 3-0 yakifungwa na wachezaji Uhuru Selemani mwenyewe,Haruna Moshi “Boban”, na Mwinyi Kazimoto.Mchezo wa leo umeisogeza zaidi Simba kuelekea kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Vodacom Bara.(Kwa hisani ya Full Shangwe).

MSANII SUMA LEE AFIWA NA MAMA YAKE

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA MUDA SI MREFU, NI KWAMBA MAMA WA MSANII SUMA LEE AMAEGA DUNIA KUTOKANA NA UGONJWA WA KIHARUSI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI,


TUMEPIGIA SIMU SUMA LEE MUDA SI MREFU YUKO MOCHWARI YA MUHIMBILI PAMOJA NA NDUGU WENGINE, LAKINI AKASHINDWA KUZUNGUMZA. taarifa zaidi zitakujia kila tutakapofanikisha kuzipata.


WAZIRI MKULO NJIA PANDA SASA!



Mapambano na ufisadi ni changamoto katika serikali ya rais Jakaya Kikwete hivi sasa kashfa zimeelekea katika wizara ya fedha na waziri mhusika ana kazi ya kueleza fuatana na gazeti la Mwananchi kuhusiana na hilo.
kashfa ya uuzwaji wa kiwanja cha Serikali namba 10 kilichoko Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL), imemuweka njiapanda Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho, uliihusisha wizara yake na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mkulo aliwahi kuingia kwenye mvutano na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe baada ya kuituhumu kamati hiyo kuhongwa ili kutetea nyongeza ya muda ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC). Kusoma zaidi bofya Read more »

UCHAGUZI DMV ULIKUWA WA KIHISTORIA!

Posted in Uncategorized on April 18, 2012
/img_9667.jpg”>Hawa ndio wajumbe ya bodi.
Bw.Jacob Merere akipiga kura yake. Kwa picha zaidi bofya Read more »

Mama Kanumba atoa ya moyoni

Posted in Uncategorized on April 18, 2012 b

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba, amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (Shiwata) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.
Kwa mujibu wa Nipashe akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na (Shiwata) jana jijini Dar es Salaam, Mama Kanumba, alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mtoto wake kila kona ya nchi.Kusoma zadi bofya Read more »

SHUKRANI ZA DHATI TOKA KWA LUVNESS

Posted in Uncategorized on April 18

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa Watanzania wote wa DMV kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huu wa uchaguzi kufika kwenu kwa wingi ndio kumefanya uchaguzi huu uwe wa kihistoria.
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote walioniunga mkono katika sera yangu ya MTANZANIA DMV BADILIKA ni jambo lakutia moyo kwa wanaDMV kusema kweli nimeguswa sana na moyo wenu wa upendo mliouonyesha kwangu, hasa timu yangu ya kampeni imefanya kazi ya ziada bila kujali muda wao.
Tatu nampongeza Iddi Seif Sandaly kwa kuchaguliwa dhidi yangu kuwa Rais wetu mpya wa Jumuiya yetu ya DMV popote pale panapo tokea mafahari wawili wanashindana lazima atokee mshindi na mshindwa kwa maana hiyo basi Ushindi wako Iddi Sandaly nimeupokea kwa mikono miwili na daima nitashiriana na wewe katika kusukuma gurudumu la maendelea DMV kama mwanajumuiya mwingine.
Mwisho, nakutakia kila la heri katika kazi yako mpya na naomba Watanzania wenzangu DMV tumuunge mkono Iddi Sandaly na uongozi wake ilikufanya kazi yao iwe rahisi. Asante na Mungu awabariki. MTANZANIA DMV BADILIKA.