amreezle

amreezle

Wednesday, March 14, 2012

 
Jay Dee hivi karibuni.
Jay Dee miezi kadhaa iliyopita.
Na Mwandishi wetu
ILE minong’ono iliyokuwa imetawala miezi kadhaa iliyopita kuwa mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jadee’ a.k.a Jide ana ‘kibendi’, imepotea baada ya hivi karibuni msanii huyo kunaswa ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni, Dar huku kitumbo chake kikiwa kimeyeyuka.
Risasi Mchanganyiko limekuwa likimfuatilia kwa karibu Jide tangu alipolazwa katika hospitali moja iliyopo Ufaransa mwishoni mwa mwaka jana.
Mara kadhaa huko nyuma Jide alieleza kwamba, alikuwa akitibiwa ugonjwa aliouita wa heri bila kufafanua zaidi.
Aidha, baada ya msanii huyo kutoa maelezo hayo, alikuwa ‘akiposti’ picha kwenye blogu yake zilizomuonesha akiwa na tumbo kubwa, kitendo kilichowafanya mashabiki wake kuanza kumpongeza wakiamini ana ujauzito.

Jide alisemaje?
Wakati wadau wengi wakitarajia kupata maelezo ya wazi kuhusiana na kilichokuwa kikimsumbua msanii huyo huku wakitaka kujua kama ni ujauzito au la, Jide alikuwa akitoa maneno ya mafumbo.
Kuna wakati ‘aliposti’ picha na kutundika maneno yasemayo ‘Behind the scene part one’ (nyuma ya pazia, sehemu ya kwanza) bila kufafanua.
Aidha, kipindi hicho mara kwa mara Jide alikuwa akitoa maneno ya kumshukuru Mungu kwa yale ambayo amekuwa akimtendea kila siku.
Sehemu ya maneno yake yalisema: “Mungu ni mkuu, amenitendea makuu… sikukata tamaa kama wengine.”


Atua nchini akiwa hana kitumbo
Katika hali iliyowashangaza wengi, wiki iliyopita Jide alitua Bongo akitokea Ufaransa kupitia Afrika Kusini na kunaswa akiwa na tumbo la kawaida.
Msanii huyo alibambwa ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge kulipokuwa na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa ‘kiwanja’ hicho ambapo aliiongoza bendi yake ya Machozi kuporomosha burudani ya kufa mtu.

Minong’ono kama kawa
Kufuatia muonekano alionao Jide kwa sasa, mashabiki wake wamekuwa wakihoji kilichotokea huku baadhi wakidai huenda lilikuwa tumbo la kawaida na sasa limepungua baada ya kufanya mazoezi na wengine wakidai eti ilikuwa ni mimba, imetoka!ila wabongo kwa kufatilia maisha ya watu.lakini ukiwa satar,lazima yatokee mambo kama hayo.by amran
 

Monday, March 12, 2012


Gumzo la jiji: Orijino Komedi maji shingoni??!!


Balotelli wa Man City akumbwa na Soo! Faini ya Sh milioni 600!

Saturday, March 10, 2012

Amran's a little dady..!

LEO KWENYE MSETO EAST AFRICA YA CITIZEN TV-10/03/12

Leo ni MOTO kwenye MSETO! JAGUAR speaks out> Listen to him as he BREAKS his long SILENCE :: Where has JAGUAR been? What is he working on after KIGEUGEU? Did he END his BEEF with PREZZO? Get all the answers as JAGUAR talks about his next PROJECT with KALAMASHAKA :: Kuna HOT HITS & 411 toka E. Africa...MZAZI nalea VIPAJI na kukugandisha kwa MAMBO MSETO (Radio Citizen 1.15pm - 4pm) LISTEN ONLINE> http://streema.com/radios/Radio_Citizen < Hapa Ndio Home!

B'Hits Studios New Release - March 2012

Hello Friends,

After the big launch ever to be hosted by a Record label in Tanzania, 
B'Hits Music is throwing its first card this year. Of course the surgeon General Mabeste is leading the postmortem once again. This time Mabeste is dropping some vulnerable lyrics reflecting the endevevours of his personal life. The little success he has attained has changed his way of life and he is promising never to go back. The song is titled "SIRUDI TENA" and it's the first time Mabeste has rhymed fast but with clarity and deep emotion on every word he is pronouncing; one could hear this from his tone. Pancho Latino as usual on his Piano is backing up the "gut spilling" session of Mabeste, and one may prefer to listen to the beat alone; No objection.

DJ CLEO AWASILI BONGO TAYARI KWA BURUDANI YA JUMAMOSI HII.

Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ Cleo Kutoka nchini Afrika ya Kusini akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere usiku huu, tayari kwa onyesho lake litakalofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam siku ya  Machi 10, 2012 siku ya jumamosi, Mwanamuziki huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake wa FACEBOOK na ameongozana na wanamuziki wenzake wawili 

Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ Cleo Kutoka nchini Afrikaya Kusini akisalimiana na Mkurugenzi wa Times FM Radio ambaye niye mwenyeji wake wakati alipokuwa akipmokea kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere. 

Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ Cleo Kutoka nchini Afrika ya Kusini katikati akiongozan na wanamuziki wenzake kwenda kupanda gari tayari kuelekea hoteli ya Protea ambako ndiko walikofikia