amreezle

amreezle

Friday, January 13, 2012


Bila shaka jina la Ali Kiba hivi sasa lipo miongoni mwa top performing artists kutoka Tanzania. Mbali ya kutoa show kali kali,Kiba amekuwa akitoa vibao ambavyo vinatokea kupendwa na kukubalika sana.Unaweza kuiita ngekewa au bahati lakini ndivyo ilivyo.Inasemekana ndiye msanii ambaye ameshafanya tour za nje ya Tanzania kuliko msanii mwingine yeyote.Anaitwa Ali Kiba,yule tule wa Dushelele,Mac Muga,Cinderella,Nakshi Nakshi,Mapenzi yana-run dunia na zinginezo nyingi.


Sasa alipokuwa katika tour yake ya Europe mwaka jana alipita katika studio za See Records zilizopo nchini Italy katika jiji la Napoli ambapo alikutana na Producer anayekwenda kwa jina la Alasko(raia wa Benin anayeishi nchini Italy). Wakaketi studio na kutengeneza kitu ambacho utakisikia punde.Wimbo unaitwa Mi Nimo…kuna maneno yanasema “Mi Nimo Najikongoja taratibu ndani ya hili shimo”…


Studio ya See Records,ambayo inatarajiwa kufungua tawi lake jijini Dar-es-salaam kuanzia mwezi Machi mwaka huu, imeshawahi kufanya kazi na wasanii wengine wengi kama vile Diamond,Hussein Machozi na pia imeshatengeneza videos za wasanii kama vile Asley Ft Mh.Temba,Tip Top Connection,Miaka 50 Mkubwa na wanae,Ramso Ft Godzilla nk.


Usikilize wimbo Mi Nimo kwa kubonyeza player hapo chini

 

Read more: BongoCelebrity

No comments:

Post a Comment