SHULE YA MAPENZI....YAFUNGULIWA AUSTRIA..!
Kwa mara ya kwanza duniani nchini Austria kwenye jiji la Vienna, imefunguliwa shule ya kufundisha kufanya mapenzi aka World’s first international applied sex school
kiasi cha paundi 1,400 itatolewa kwa mwanafunzi atakayekaa hostel ambapo watakua wanafanya homework kabisa na Ylva-Maria Thompson, mkuu wa chuo hicho amefunguka kuwa elimu itakua inatolewa kivitendo zaidi
RAPPER DMX....AVAMIWA KWENYE STAGE...!
Rapper DMX,amepata msala alipokua anapiga show pande za Cafe Sevilla,Long Beach-California baada ya fan wake mmoja kuruka kwenye stage na kumvaa Wakati DMX anaanza kuimba track yake ya One More Road to Cross iliyokua kwenye album yake ya 3 aliwauliza fans wake "Are you ready to get this shi* started for real?....ndipo jamaa alivamia stage na na kumkaba shingoni kabla ya security kumuokoa DMX na mumtoa kwenye stage
MOVIE YA KENYA....YAPATA SHAVU MAREKANI...!
Filamu fupi toka Kenya imechaguliwa kushiriki kwenye Manhattan International Film Festival baadaye mwaka huu
Filamu hiyo inaitwa Brother-Brother chini ya Producer/Director Sheila Mulinya itaoneshwa kwenye Festival jijini New York,kuanzia tarehe 27 na 28 June,2012 Na ikishinda top 3 itaoneshwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na filamu ya Brother-Brother ni story inayowahusu ndugu wawili pande za Kawangware,Nairobi na ilitengenezwa August 2008
MONICA NA BRANDY.....KUPIGA MZIGO PAMOJA 2012...!
Baada ya kutoa bonge la collabo na Brandy iliyoitwa The Boy is Mine iliyokua kwenye studio album yake ya 2 iliyoitwa The Boy is Mine mwaka 1998,Kwa sasa Monica na Brandy wako kwenye mishe za kufanya kazi tena pamoja
MONICA DENISE BROWN
Brandy na Monica wako kwenye mazungumzo na Producer Rico Love ili waingie studio,na haijajuliaka na kama watatoa single au joint album.... Just let's wait & See!
ELTON JOHN....AMPA SHAVU TIMBERLAKE...!
Mkongwe wa Muziki toka Uingereza,Sir Elton John amefunguka kuwa ana mpango wa kumshirikisha Artist Justin Timberlake kwenye 'Biopic' yake aka movie inayohusu life story yake
JUSTIN RANDALL TIMBERLAKE
Kwa sasa kila kitu kiko kwenye mstari,na Director na crew nzima iko tayari wanasubiri script tu waanzae mambo na movie hiyo itakua na track zake mpya na Justin Timberlake,amekua chaguo lake la kwanza coz alisha act kwenye video ya Elton John ya David LaChapelle ‘Rocket Man’ na Elton john amechaguliwa kuwania tuzo kwenye Golden Globe zitakazofanyika January 15,2012 kupitia track yake ya Hello, Hello na ana mtoto wa kuasili yeye na 'husband wake' David Furnish aitwaye Zachary,aliyezaliwa December 25,2010
RAPPER JAY Z NA LUDACRIS....BEEF KIMTINDO...!
Imefunguliwa kuwa Baba Ivy Blue Carter aka Jay-Z wako kwenye ka-beef cha kiaina na Hip Hopper, Ludacris kuhusiana na kugombea eneo la biashara pande za Atlanta
SHAWN COREY CARTER - JAY Z
Jay-Z na Ludacris walikua wanawania sehemu pande Hartsfield-Jackson Airport-Atlanta,lakini airport hiyo ilikua na uwezo wa kumpangisha mtu mmoja na hatimaye Ludacris akalamba deal hiyo na kuamua kufungua Restaurant iitwayo Chicken N Beer
Sunday, January 8, 2012
JAY-Z NA BEYONCE.....WAPATA BABY GAL...!
Artist Beyonce Jigga Knowles na Rapper Jay Z,baada ya kuwa na uhusiano kwa miaka 6 na kufunga ndoa rasmi April 2008,wamepata motto wa kike waliyembatiza jina la Ivy Blue Carter jijini New York
Imefunguliwa kuwa Beyonce alijifungua pande za Lenox Hill Hospital,Ijumaa usiku baada ya kukodi ghorofa ya 4 sehemu ya hospitali hiyo kwa dola milioni 1.3 za kimarekani
Kabla ya kujifungua ma-doctor na ma-nurse wa hospitali hiyo walikatazwa kufika ghorofa ya 4 na wale waliokua pande hizo walinyanganywa simu zao ili wasiweze kupiga picha wakati Beyonce akijifungua
Friday, January 6, 2012
RIHANNA....BEST SELLING ARTIST ONLINE 2011...!
R & B Star,Robyn Rihanna Fenty aka Rihanna amevalishwa taji la Queen wa kuuza mziki kwenye mtandao aka Best selling artist online
Ofisa toka kampuni ya Nielsen SoundScan amefunguka kuwa fans wali- download track za Rihanna mara milioni 47.5 kufikia mwisho wa mwaka 2012
Kundi la Black Eyed Peas limepata downloads milioni 42.4 kupitia track yao ya I Got Feeling huku Eminem wa 3 kwa kupata downloads milioni 42.2 na Lady Gaga ni wa 4 kwa kupata downloads milioni 42 na Taylor Swift downloads milioni 41.8
Pia artist Katy Perry,Lil Wayne,Beyonce,Kanye West na Britney Spears wamo kwenye Top 10
NAS....AZINGUA ANGOLA....AZUSHA MSALA...!
Nasir bin Olu Dara Jones aka Rapper Nas Escobar amezingua nchini Angola na kusababisha Promoter wa show hiyo atekwe nyara
Nas ilikua akapige show 2 siku ya mkesha wa mwaka mpya nchini Angola chini ya udhamini wa AllGood Entertaiment,na kusababisha Mkurugenzi wake,Patrick Allocco na mtoto wake wa kiume kutekwa nyara na majambazi wenye silaha waliokodiwa,kwa kua Nas hakwenda kupiga showz
Lakini Rapper Nas ameahidi kurudisha mkwanja wa $ 315,000 za kimarekani aliopewa ili apige show na alifunguka kuwa alishindwa kwenda Angola baada ya kutoelewa kuhusu usafiri
P-UNIT....WAPATA SHAVU LA LAPTOP ZA HP...!
Kundi la P-Unit toka Kenya walitarajiwa kupata shavu la kutangaza laptop za HP kwenye kampeni iliyobatizwa jina la 'Get your beat On' ambazo mteja akinunua anapata na headphones kali za Beats by Dre
P-Unit wameungana na international artistes ambao walipata shavu kama hilo kama David Guetta,Alicia Keys,Justin Bieber,Sean ‘Diddy’ Combs,Lebron James na Lady Gaga
BEYONCE NA JAY - Z....WASABABISHA MSALA....!
Celebz,Jay Z na Beyonce bila kujijua walisababisha shabiki wao mmoja kuchomwa kisu pande Ohio – Marekani baada ya kutokea mabishano juu yao
RONALD DEAVER
Issue ilianza baada ya jamaa mwenye miaka 48 kubishana na jamaa anayekwenda kwa jina la Ronald Deaver mwenye miaka 31,kwa kua alikua hana habari kama Beyonce ameolewa na Jay Z na mpaka kuwa na 'kitumbo' ndipo kulisababisha Ronald kumchoma kisu na kupelekea kukamatwa na maafisa polisi wa Ohio nchini Marekani
BIG BROTHER AFRICA-2012....KUANZA MWEZI MAY...!
Reality show maarufu ya Big Brother Africa inatarajia kuanza mwezi May, 2012 nchini Afrika Kusini
Shindano hilo linadhaminiwa na Coca-Cola na Endemol South Africa kupitia M-Net na itakua ni season ya 7 na mshindi mmoja tu atapatikana na waandaaji wamefunguka kuwa wameanza kupokea washiriki wanaotaka shavu kwa mwaka huu na kufunguka zaidi kuwa wanataka kufanya mambo makubwa sana kwenye historia ya Big Brother Africa
MKE WA BEBE COOL.....KUZALIA MAREKANI..!
Zuena Kirema aka Mrs Bebe Cool toka Uganda ambaye anatarajiwa kujifungua twins anatarajiwa kuelekea nchini Marekani kwenda kujifungua
Za chini ya Carpet zinadai kuwa Bebe Cool miezi 3 nyuma alikua kwenye mishe mishe za kutafuta visa na nia yake ni kupata watoto ambao watazaliwa Marekani na kupata uraia,na pia awe kwenye mikono salama ya Mama yake Bebe Cool anayeishi Marekani
Thursday, January 5, 2012
RAIS OBAMA.....AJIACHIA KAMA KAWA....HAWAII..!
Rais wa Marekani,Barack Obama amebambwa na mtandao wa kimbea zaidi duniani akicheza american football,akiwa ametupia kapelo,pensi na akiwa tumbo wazi pande za Visiwa vya Hawaii
Rais Obama alikua kwenye mapumziko ya siku 10 ya mwisho wa mwaka yeye na familia yake kwenye kambi ya Kaneohe Marine Corps Base na alionekana akidaka mpira na kujiachia kwenye michanga kama kawa na alirejea hivi karibuni nchini Marekani baada ya holiday na kuanza mishe mishe za kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 6,2012
RAPPER DRAKE....MWAKA MPYA,DEMU MPYA...!
Baada ya kutokea uvumi kuwa anatoka na BasketBaller wa New Jersey Nets,Kris Humphries,Model Dollicia Bryan amefunguka kuwa yeye ndio queen mpya wa Drizzy Artist toka Young Money na si Kris kama inavyodaiwa
DRAKE vs DOLLICIA BRYAN
Kris Humphries alikua mume wa Model/Actress/TV personality Kimberly 'Kim' Kardashian aliyekua na beef na Dollicia na Mwakilishi wa Dollicia Bryan alifunguka kuwa kwa sasa shosti huyo anatoka na Drake na kwa sasa wako pande za Los Angeles wakila bata kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka na kabla ya kutoka na Drake,Dollicia Bryan alikua 'anatoka' na actor Hill Harper
KOBE BRYANT.....AICHAKACHUA NDOA YAKE...!
BasketBaller Kobe Bryant toka Los Angeles Lakers imefunguliwa kuwa ameichakachua ndoa yake kwa kutembea nje ya ndoa
KOBE & VANESSA BRYANT
Inadaiwa kuwa NBA star Kobe Bryant amemchakachua wife wake Vanessa Bryant aliyezaa nae watoto 2,kwa kutembea na wanawake wapatao 105 katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yao
....KOBE BRYANT FAMILY....
Vanessa alimkodi mtu kumpeleleza Kobe Bryant na inasemekana ameshakula uroda na rafiki wa Kim Kardashian,Carla DiBello,Playboy model Jessica Burciaga na actress Sanaa Lathan na kwa sasa Vanessa amewasilisha madai ya talaka na kwa mujibu wa sheria za California, mali zilizochumwa wakati wa ndoa hugawiwa nusu kwa nusu na utajiri wa Kobe Bryant unakadiriwa kufikia $ milioni 200
ARETHA FRANKLIN....KUOLEWA NA MIAKA 69....?!
Mkali wa muziki wa Soul toka Marekani,Aretha Loiuse Franklin mwenye umri wa maiak 69 amechumbiwa na long time friend wake William 'Willie' Wilkerson
Aretha Franklin ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy alivalishwa pete na Wilkerson wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka na kwa sasa mipango ya harusi inafanyika pande za Miami Beach,Florida na Bibi Aretha Franklin ana mpango wa kufanya sherehe ya watu wake wa karibu tu kwenye boti na anafikiria ma-designer kama Vera Wang,Valentino na Donna Karan wamtengenezee gauni lake la harusi na hii itakua ni ndoa yake ya 3 baada ya kuolewa mara 2 kabla
WADOSI WAMZINGUA....FOOTBALLER JOHN TERRY...!
Mwakilishi wa Footballer toka Chelsea na England,John Terry ametishia kuishitaki serikali ya India baada ya kutoa tangazo la sigara lenye picha inayofanana na sura ya John Terry
....TANGAZO LA SIGARA....
Taswira ya John Terry imetokea kwenye tangazo la sigara za Gold Flake, zikisema "smoking kills" na haijajulikana mpaka sasa ilikua mpaka picha hiyo ikatimika na hii si mara ya kwanza kwa nchi ya India kuzingua coz Jimbo la Meghalaya nchini humo walitoa madaftari ambayo yalikua na picha ya yesu ameshika kopo la bia na sigara
RICK ROSS.....AZINGUA NIGERIA...AKOMALIWA!
Serikali ya Nigeria ina mpango wa kumshitaki Rapper toka Marekani,William Leonard Roberts II aka Rick Ross baada ya kushindwa kutia maguu na kupiga show kwenyetamasha maarufu la The Calabar Christmas Festival pande za Cross River State
Imefunguliwa kuwa Rick Ross alishakula mkwanja wake na haijajulikana sababu ya kutokwenda kupiga show serikali ya Cross River State kwa sasa imekodi mwanasheria toka Marekani kwa ajili ya kumfungulia mashitaka Rick Ross
NICK CANNON....AKIMBIZWA HOSPITALI....!
Mume wa Artist Mariah Carey,Artist Nick Cannon amekimbizwa hospitali pande za Aspen baada ya kupata matatizo ya figo
Nick Cannon alianza kupata matatizo wakati wa pambano la boxing la Amir Khan wiki chache zilizopita na Mariah Carey alitupia kwenye mtandao wa twitter kuwataka fans wake wamuombee husband wake apone haraka na kwa sasa inasemekana kuwa anaendelea poa tu!
Tuesday, January 3, 2012
CHRIS BROWN vs RIHANNA...KURUDIANA 2012..?!
ARTIST WA UGANDA....WAFANYA REMIX YA WINDECK...!
Artist toka Uganda wamefanya remix ya hit track ya Artist toka Angola,Cabo Snoop ya Windeck
Artist Navio,Peter Miles na Airport Taxi Crew inayoundwa na rappers,William na Tucker na female vocalist Martha na wamegonga Remix hiyo ambayo imefanyika jijini Kamoala-Uganda kwenye studio ya Talent Africa,chini ya Producer Samurae
ARTIST J. MARTINS WA NIGERIA....AFUNGA NDOA ..!
Artist na Producer toka Nigeria,Joshua Kalu Okwun aka J. Martins amefunga ndoa na longtime girlfriend,Nnezi Mbila jana January 2,2012
J. Martins alifanya sherehe ya kimila pande za Ohafia,Abia State ambayo ilihudhuriwa na wanafamilia,marafiki wa karibu
J. Martins ni mmoja kati ya majembe yaliyowaweka wasanii P-Square kwenye ramani ya muziki duniani coz amefanya production asilimia kubwa ya hit songs zao na mpaka yeye mwenyewe kuamua kutoka kivyave kwa hits kama Oyoyo,Iva,Jukpa nk
STL....ACHUMBIWA...KUPIGA TOUR AFRICA 2012..!
Stella Mwangi aka STL,Artist toka Kenya anayeishi nchini Norway amefunguka kuwa amevalishwa pete ya uchumba aka she is engaged na mtu ambaye si mwana muziki na soon atakua ni mke wa mtu
....KITU CHA PETE....
STL msimu wa Christmas alikua nchini TZ na kufanya remix collabo ya moja ya ngoma zake na Artist Ambwene Yessayah aka AY na kwenda ncihin Uganda alipokwenda kuandika lyrics na Hip Hopper toka Uganda,Navio na Rich Richie,ameonekana na pete ya dhahabu ikiwa featuring almasi kidogo na amefunguka kuwa mwaka 2012 ana mpango wa kufanya African Tour na alikua Afrika Mashariki kimuziki zaidi
Subscribe to: Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment