amreezle

amreezle

Wednesday, March 14, 2012

 
Jay Dee hivi karibuni.
Jay Dee miezi kadhaa iliyopita.
Na Mwandishi wetu
ILE minong’ono iliyokuwa imetawala miezi kadhaa iliyopita kuwa mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jadee’ a.k.a Jide ana ‘kibendi’, imepotea baada ya hivi karibuni msanii huyo kunaswa ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Kinondoni, Dar huku kitumbo chake kikiwa kimeyeyuka.
Risasi Mchanganyiko limekuwa likimfuatilia kwa karibu Jide tangu alipolazwa katika hospitali moja iliyopo Ufaransa mwishoni mwa mwaka jana.
Mara kadhaa huko nyuma Jide alieleza kwamba, alikuwa akitibiwa ugonjwa aliouita wa heri bila kufafanua zaidi.
Aidha, baada ya msanii huyo kutoa maelezo hayo, alikuwa ‘akiposti’ picha kwenye blogu yake zilizomuonesha akiwa na tumbo kubwa, kitendo kilichowafanya mashabiki wake kuanza kumpongeza wakiamini ana ujauzito.

Jide alisemaje?
Wakati wadau wengi wakitarajia kupata maelezo ya wazi kuhusiana na kilichokuwa kikimsumbua msanii huyo huku wakitaka kujua kama ni ujauzito au la, Jide alikuwa akitoa maneno ya mafumbo.
Kuna wakati ‘aliposti’ picha na kutundika maneno yasemayo ‘Behind the scene part one’ (nyuma ya pazia, sehemu ya kwanza) bila kufafanua.
Aidha, kipindi hicho mara kwa mara Jide alikuwa akitoa maneno ya kumshukuru Mungu kwa yale ambayo amekuwa akimtendea kila siku.
Sehemu ya maneno yake yalisema: “Mungu ni mkuu, amenitendea makuu… sikukata tamaa kama wengine.”


Atua nchini akiwa hana kitumbo
Katika hali iliyowashangaza wengi, wiki iliyopita Jide alitua Bongo akitokea Ufaransa kupitia Afrika Kusini na kunaswa akiwa na tumbo la kawaida.
Msanii huyo alibambwa ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge kulipokuwa na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa ‘kiwanja’ hicho ambapo aliiongoza bendi yake ya Machozi kuporomosha burudani ya kufa mtu.

Minong’ono kama kawa
Kufuatia muonekano alionao Jide kwa sasa, mashabiki wake wamekuwa wakihoji kilichotokea huku baadhi wakidai huenda lilikuwa tumbo la kawaida na sasa limepungua baada ya kufanya mazoezi na wengine wakidai eti ilikuwa ni mimba, imetoka!ila wabongo kwa kufatilia maisha ya watu.lakini ukiwa satar,lazima yatokee mambo kama hayo.by amran
 

No comments:

Post a Comment