amreezle

amreezle

Wednesday, November 9, 2011

MIMBA YA WEMA YAWA KERO



WEMA Isaac Sepetu (pichani), mwenye kibendi cha miezi miwili kasoro alichopachikwa na ‘kidume’ Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, amegeuka kero kwa baadhi ya mastaa Bongo hasa wa kike kutokana na kutema mate ovyo, kujichetua na kuinadi mimba yake kupita maelezo.

Akizungumza na The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema alisema kuwa kinachosababisha awe kero ni dalili za wazi za mjamzito alizonazo ikiwemo kutema mate ovyo, kubagua vyakula na kudeka kupitiliza.

Alifunguka: “Wanasema nawakera, lakini nahisi wananionea gere na mimba yangu. Mimi sina chuki na mtu yeyote na naomba wanivumilie.”

MWANAMUZIKI DOGO ASLAY ALIVYOTAMBULISHWA DAR

MWANAMUZIKI mwenye umri mdogo anayetokea pande za Temeke, jijini Dar es Salaam,  Aslay Isiaka, ambaye ameibuliwa na kundi la Mkubwa na Wanawe linalomilikiwa na Said Fella, jana alitambulishwa rasmi  kwa wanamuziki wengine katika viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Utambulisho huo ulihudhuriwa na wanamuziki wengi mahiri wakiwemo wa kundi la Tip Top Connection likiongozwa na ‘Rais wa Manzese’, Hamadi Ally ‘Madee’, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Sumalee,,Tunda Man na kundi zima la TMK.

- SIKILIZA WIMBO MPYA WA MWANAMUZIKI DITTO KUTOKA THT -JINA LA WIMBO NI TUSHUKURU KWA YOTE -PRODUCED AND MASTERED BY MSWAKI AT HOMETOWN RECORDS


No comments:

Post a Comment