amreezle

amreezle

Monday, May 7, 2012

Washindi wa tuzo za Kili Awards wapagawisha Mwanza

Posted in Uncategorized on May 7, 2012 
Mkali wa Bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza Jumapili.
Wasanii wa Musiki wa Kizazi Kipya Diamond, Roma, Isha Mashauzi, AT, Barnaba, Omy Dimpoz, Ben Paul wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza, na kutoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa burudani ya Muziki wa jiji hilo na vitongoji vyake.
Show hiyo kali iliyoanza majira ya saa 8 mchana ikitanguliwa na makundi kadhaa ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva wa Jijini Mwanza ilizidi kupamba moto muda hadi muda hadi pale wasanii Nguli na washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 walipowasili uwanjani hapo.Kusoma zaidi bofya Read more »

No comments:

Post a Comment