amreezle

amreezle

Wednesday, May 30, 2012


Video ya ‘No Church in the Wild’ ya Kanye West na Jay-Z yatoka ikiwa na ujumbe mzito

Hatimaye video ya wimbo mpya wa Kanye West na Jay-Z, “No Church in the Wild” jana imetoka. Video hiyo inawaacha mashabiki na ujumbe mzito hata kama nguli hao wawili hawaonekani kwenye video. Kwa mujibu wa MTV uamuzi huo wa Kanye … Continue reading

Facebook kuanza kutengeneza simu kama iPhone!!


Theluthi ya watumiaji wa simu wako tayari kununua simu ya Facebook (smartphone) na asilimia 73 wanadhani wazo la mtandao huo kuwa na simu zake ni zuri.
Habari za simu hiyo zimeibuka wiki hii huku vyanzo vikidai kuwa Facebook imemwajiri engeener wa zamani wa Apple kutengeneza simu ‘rasmi’ ya Facebook.
Sio mara ya kwanza kwa simu za Facebook kuingia sokoni.
Mtandao huo wa kijamii uliwahi kuingia ubia na makampuni ya INQ na HTC kutengeneza simu za Facebook zikiwemo simu zilizowekewa button ya ‘Like’ ndani.
Simu hiyo inasemekana itakuwa tayari kuzinduliwa rasmi mwaka ujao.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na MyVoucherCodes kwa kuhoji watu 968, asilimia 32% wamesema watainunua ikiwa tayari.
Asilimia 57 wamesema wanaamini simu hizo zitakuwa na bei nafuu kuliko iPhone.
Baada ya iphone kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Samsung Galaxy, Facebook kuwa mpinzani mwingine mwenye nguvu? Yetu masikio.

Will Smith: Nina bahati Jada kuwa mke wangu


Will Smith amemsifia mke wake Jada Pinkett kwa kuifanya familia yake kuwa pamoja.
Muigizaji huyo wa Men In Black III na mke wake muigizaji wa series ya Hawthorne wana miaka 17 tangu waoane licha ya hivi karibuni kuwepo na fununu kuwa ndoa yao ipo matatani kuvunjika. Continue reading
Posted in Will Smit

No comments:

Post a Comment