Dj Fetty Apata Deals Baada Ya Kupiga Show Big Brother Africa
Kwa fans wote wa Big Brother Africa najua kama ulipata chance ya kuchek show weekend iliyopita najua sina haja ya kuuliza trending topic kwenye mitandao ya kijamii ilimuhusu nani.
Ofcourse my girl Fetty the best Dj Fetty wa XXL ya CLOUDS FM ndio alikua Dj aliepewa mwaliko wa kuonyesha ujuzi jumamosi na jumapili.
Kwa show hizo mbili tu alizopiga hakika Africa imemtambua ambapo tayari watu kadhaa wameweka wazi nia ya kutaka kufanya nae kazi.
Exclusive na millardayo.com Fetty amesema baada ya show alifatwa na Channel O, kituo cha Television cha South Africa chenye heshima kwenye burudani ambapo kimetaka awe Dj kwenye show yao maarufu ya usiku ya Basement.
Fee’h amesema yuko nao kwenye mazungumzo ambapo atatoa matokeo soon, vilevile amepata mialiko ya nchi kadhaa za Africa kwa ajili ya kwenda kupiga kama Dj ambapo nchi ya kwanza kumtumia maombi asubuhi yake baada ya kupiga show ni Rwanda, bado hajawajibu mpaka sasa anavuta subira kidogo alafu afunguke…. kama kutakua na any news… utakua wa kwanza kuifahamu kupitia millardayo.com!
No comments:
Post a Comment