Photos: Usiku wa Kili Music Awards Winners Tour-Dar
Bongo Star Search: Shindano linalotoa washindi wasiomudu ushindani wa muziki
Mwaka huu Bongo Star Search imekuja na kasi mpya. Ikiwa na wadhamini wapya sasa hivi inajulikana kama Epiq BSS. Udhamini huo mnono unaambatana na kitita cha shilingi milioni 50 zitakazotolewa kwa mshindi wa mwaka huu.
Harufu inayodhihirisha kuwa mashindano ya mwaka huu yanaweza kuwa na utofauti mkubwa imeshaanza kunukia. Kwanza kwa matangazo yanayovutia yaliyoandaliwa na wadhamini, yanayosikika kwenye vituo vya radio na kuamsha hamu ya watazamaji wa TV wanayoyasubiria. Continue reading
Evander Holyfield kwenda jela kama asipotoa hela ya matumizi kwa mtoto!
Bondia mkongwe Evander Holyfield anaweza kukabiliwa na kifungo jela kama asipotoa takriban $300,000 kama fedha za matumizi kwa mwanae.
Bondia huyo hajatoa fedha hizo kwa ajili ya mwanae wa kike Emani,18, tangu April 2010 alipoamriwa na mahakama kufanya hivyo.
Na sasa anadaiwa $372,097.40.
Msemaji wa Evander ameuambia mtandao wa TMZ kuwa hakuwa na taarifa kuhusiana na jambo hilo na kuongeza kuwa, “Holyfield ana uhusiano mzuri na binti yake.”
Hata hivyo ‘Upendo haulipi bili’. Toa hela!
Baada ya Fishcrab,producer Lamar aja na Filmatic
Producer na mshindi wa tuzo za Kili Lamar wa Fishcrab ameamua kuonesha kuwa si uandaaji wa muziki pekee anaouweza bali kamba yake ni ndefu zaidi ya hapo ilipomfikisha.
Mpishi huyo wa midundo ya ukweli nchini, amefungua kampuni mpya chini ya himaya yake ya Fishcrab iitwayo Filmatic.
Akiwa muongozaji mkuu na mchukua picha, mpaka sasa Lamar na timu nzima ya Filmatic ameshatengeneza video tano.
Jana kupitia ukurasa wa Twitter alisema Continue reading
Licha ya kwenda jela, pambano la dhidi ya Mayweather na Pacquiao lanukia
Juzi bondia Floyd Mayweather alijisalimisha mwenyewe jela huko Las Vegas kutumikia kifungo cha siku 87 kutokana na kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani mbele ya watoto wao.
Hata hivyo hatua hiyo haijaathiri pambano linalongojewa kwa hamu kuliko yote kati yake na mfilipino Manny Pacquiao. Habari njema ni kuwa mabondia hao sasa hivi wanazungumza moja kwa moja.
Kwa mujibu wa mwalimu wa Pacquiao Freddie Roach pambano hilo linanukia.
“Golden Boy (promota wa Mayweather) na (Arum, promota wa Pacquiao) wanachukiana kiasi ambacho wameamua kukaa pembeni. Kwahiyo Manny na Floyd wameanza kuongea wenyewe, ” alisema Roach.
“Watagawana 40-40 na mshindi atachukua hela ya ziada. Kitu ambacho ni sawa sababu kila mmoja anasema atashinda.”
Wakazi aja na kanuni kumi za hela
Ukimuuliza Fid Q ni rappers gani anaowakubali zaidi Tanzania hawezi kukosa kumtaja Webiro Wasira aka ‘Wakazi’. Kama Fid kamkubali hatuna shaka kuwa uwezo wake si haba.
Jamaa anatokea pande za Ukonga, Dar es Salaam lakini kwa muda mrefu sana anaishi Chicago, Illinois nchini Marekani.
Katika ulimwengu wa Hip Hop wakazi ni mfalme wa kanda mseto (mixtape). Mpaka sasa ameshaachia mixtape tatu, MYU: Mixtape Ya Ukweli, MYU2 The Return of The Bilingual Beast na MYU3 Welcome To Heartbreak.
Jumapili hii amekuja na kanuni kumi za hela alizoziweka kwenye vina, ambazo ni hizi zifuatazo:
Continue reading
Lady Jaydee ni mtu wa tatu maarufu zaidi Tanzania kwenye mtandao
Kwa mujibu wa mtandao wa starcount.com, leo Judith Wambura aka Lady Jaydee ni mtu wa tatu maarufu zaidi nchini Tanzania kwenye mitandao ya kijamii.
Mtandao huo uliozinduliwa rasmi juzi (May 31) ni mkubwa zaidi wa aina hiyo wenye uwezo wa kusoma tabia za watu bilioni 1.5 duniani kote. Continue reading
Misimamo yake ROMA ilimfanya afukuzwe shule
Ibrahim Musa aka Roma kama watu wanamvyomtambua, hakuanza leo hii kuwa na misimamo mikali dhidi ya utawala.
Msimamo mkali ulimcost masomo pamoja na wenzake kadhaa baada ya kufukuzwa shule alipokuwa katika shule ya Sekondari ya Old Moshi.
Continue reading
Freemason: Dhana inayopanda mbegu ya ujinga na uvivu kwa vijana wa Tanzania
“Jamaa ana nyumba mbili Mbezi Beach, ana gari tatu na maduka mawili makubwa, aah yule ni Freemason mwanangu, haiwezekani avipate hivi hivi”!! Huo ni mfano wa kauli za aina hiyo zilizogeuka kuwa maarufu sana kwenye midomo ya watanzania.
Continue reading
Wahu akanusha kumuimbia mumewe kwenye ‘Liar”
Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya Wahu amezikanusha story kuwa amemlenga mumewe kwenye wimbo wake Liar.
Kwa muda mrefu wapenzi wa muziki nchini humo wamekuwa wakihisi kuwa anayeambiwa ‘mwongo’ kwenye ngoma hiyo ni mume wake David Mathenge, aka Nameless, ambaye ni maarufu sana kwa mashabiki wa kike.
Katika interview aliyofanya na kituo cha radio cha Easy FM Wahu amesema kisa hicho ni cha kutunga.
“Kila mtu anaendelea kusema, aya, maze sema tu ukweli, you know. (The liar) ni uhusika wa kutunga lakini unaozungumzia mambo yanayotokea. Si unajua watu ni waongo,” alifafanua.
Wimbo huo kutoka kwa mshindi huyo wa tuzo za MTV, Wahu Kagwi umetengenezwa na producer maarufu
Tyrese: Nahitaji kufanya movie nyingine na Taraji
Unaikumbuka filamu maarufu sana ya Baby Boy (2001) aliyoigiza mwanamuziki Tyrese, rapper Snoop Dogg na muigizaji maarufu Taraji P Henson?
Katika filamu hiyo Tyrese ameigiza kama Jody (20) anayeishi na mama yake Juanita. Tyrese ameigiza kama mtoto wa mama fulani ambaye haoneshi dalili ya kuwa mtu mzima na kukabiliana na majukumu kama baba baada ya kumzalisha mpenzi wake Yvette (Taraji P. Henson) mtoto wa kike aitwaye Peanut.
Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakisubiri sana ujio mpya wa filamu nyingine itakayowakutanisha wawili hao. Leo (June 2) Tyrese kupitia Twitter ameonesha kuwa yeye pia ana hamu ya kukutana na Taraji. “I need to do another movie with this woman …. Fast … Where is my baby.?” Ametweet akiambatanisha picha waliyopiga pamoja.
Tweet hiyo inatupa maswali mengi hasa anapoandika’ Fast’ kwasababu tunajua kuwa awamu ya sita ya filamu maarufu ya Fast and the Furious ambayo Tyrese yumo kwenye zote tano zilizopita, huenda Taraji akaonekana humo pia! You never know!
Mwezi July mwaka jana Tyrese alitweet pia kwa kuandika, “Official.. Me and my girl Taraji are doing another classic together soon.!! John Singleton will be directing us. And it’s not BB2.”
Vyovyote itakavyokuwa, Taraji na Tyrese wanapendeza sana kuwa kwenye movie moja.
No comments:
Post a Comment