amreezle

amreezle

Tuesday, June 19, 2012

Taarifa za kutatanisha kuhusu hali ya Hosni Mubarak -CNN

Posted  on June 19, 2012 by amran


Kiongozi wa Misri Hosni Mubaraka atangazwa yu mahututi na pengine amefariki Dunia. Alikuwa kwenye mashine za kupumulia lakini inasemekana pia zimeondolewa.Hali halisi bado ya utata.

BIG BROTHER STAR GAME EVICTION

Posted  on June 19, 2012 by amran
The 91 day reality super-series Big Brother StarGame, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv channel 197 & 198. Last night (Sunday 17 June) Lee & Jesica were evicted while Junia & Keagan upgraded to Upville. For more information log on to www.africamagic.tv/bigbrotherr Pictured here: Tanzania’s AY.

Lulu akwama kupanda kizimbani

Posted  on June 19, 2012 by amran

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji jana amefikishwa mahakamani na kurejeshwa tena mahabusu bila kupandishwa kizimbani.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kumuua aliyekuwa muigizaji nyota wa filamu Tanzania, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba.
Jumatatu, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kutajwa, lakini hakupandishwa kizimbani na badala yake alirudishwa tena mahabusu katika gereza la Ukonga.Kusoma zaidi bofya Read more »

Migiro awataka Watanzania kuchapa kazi kwa nidhamu

Posted  on June 19, 2012 by amran

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro amewaasa Watanzania kufanya kazi kwa bidii na nidhamu kupata mfanikio katika sekta yoyote ile.
Amesema hakuna jambo njema katika utumishi wowote ule uwe wa kuajiriwa serikalini ama sekta binafsi au hata kujiajiri mwenyewe kama utafanya kazi kwa bidii na nidhamu.
Migiro alitoa kauli hiyo wakati akisalimiana na Watanzania waliopo New York, Washigton DC na vitongoji vingine wakati wa hafla ya kusherehekea mafanikio yake ya kushika wadhifa wa Unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Miaka mitano na nusu. Kusoma zaidi bofya Read more »

Mbunge amlipua mfanyabiashara kwa ujasusi

Posted  on June 19, 2012 by amran

Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed jana aliilipua Kampuni ya Madini ya Minerals Extractions Technologies Ltd kutokana na mmiliki wake kufanya biashara za madini kwa njia za utapeli na ujasusi.
Minerals Extractions Technologies Ltd ni kampuni ambayo inafanya kazi ya kusafisha mchanga wa dhahabu katika baadhi ya migodi iliyopo Kanda ya ziwa na iliwahi kulalamikiwa kwa kukataa kushirikiana na mpango wa kufuatilia mapato yanayolipwa kwa Serikali na kampuni za madini, gesi na mafuta (TEIT) unaoongozwa na Jaji Msitaafu, Mark Bomani.
Kutokana na hali hiyo, Mohamed alitoa mapendekezo ya kuundwa kwa kamati ya wabunge sita kutoka Kamati tatu za Bunge ili kuchunguza kampuni hiyo na mmiliki wake ambaye (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye alisema kuwa anatamba kwamba Tanzania hakuna mtu anayeweza kumgusa. Kusoma zaidi bofya Read more »

BAADA YA SAKATA LA KUTOLEWA BUNGENI MNYIKA AZUNGUMZA NA VOA.

Posted  on June 19, 2012 by amran

Baada ya mbunge John Mnyika alizungumza na VOA juu ya sakata la kutolewa nje ya bunge.kUSIKILIZA MAHOJIANO HAYO BOFYA HAPA.


John Mnyika atolewa nje ya bunge

Posted  on June 19, 2012 by amran
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea. KWA HISANI YA FULLSHANGWE.

Polisi wa Uganda wazuia mkutano wa mashoga

Posted  on June 19, 2012 by amran

Polisi nchini Uganda Jumatatu jioni waliivunja warsha ya siku tatu ya wapenzi wa jinsia moja wakisema mkutano huo ulikiuka sheria kwa sababu wapenzi wa jinsia moja hawatambuliwi na sheria. Watu wanne akiwemo waandalizi wa mkutano huo walitiwa mbaroni.
Mkutano huu ulikuwa unahudhuriwa na washirika 20 kutoka nchi ya Rwanda, Tanzania, Kenya na Uganda. Kila nchi ikiwa imechangia washiriki watano.
Kwa mujibu wa VOA Njoroge Waithera kutoka Kenya ni miongoni mwa watu waliokuwa wanahudhuria mkutano huu. Mwandishi wa Sauti ya Amerika alimuuliza kama mkutano huu ulikuwa wa wapenzi wa jinsia moja.Kusoma zaidi bofya Read more »


No comments:

Post a Comment