Kishido cha bajeti kuunguruma Tanzania..!!
Posted on June 15, 2012 by amranWaziri wa fedha Tanzania Dr.Mgimwa akizungumza na waandishi.
Alhamisi ni siku ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2012/13. Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa anatarajiwa kuanza kusoma Bajeti ya Serikali inayosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya Wananchi 10.00 jioni saa za Afrika Mashariki.
Hotuba ya Dk Mgimwa itatanguliwa na ile ya Mipango ya Serikali itakayosomwa asubuhi mara baada ya kipindi cha Maswali na Majibu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira.
Kutwa nzima ya Jumatano, Dk Mgimwa na watendaji wengine wa Wizara ya Fedha walikuwa katika pilikapilika za kukamilisha maandalizi ya bajeti hiyo ya Sh15 trilioni, ambayo inatarajiwa kuwa na vipaumbele saba.Kusoma zaidi bofya Read more »

WAIGIZAJI FILAM WAFURAHISHWA NA KUFANYIKA TUZO ZA FILAM MWAKA HUU:
Posted on June 15, 2012 by amreezleMwigizaji wa filamu Irene Uwoya akiongea mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutangaza tuzo za filamu zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini TUZO hizo za kwanza kabisa za waigizaji wa filamu zimepangwa kufanyika mwezi ujao, Mratibu wa kampuni ya Bantu Film Award, Stuart Kambona amesema, Mkutano huo umefanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Mwigizaji Irene Uwoya amewapongeza waandaaji hao kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo alisema zitawapa changamoto kwao kuandaa filamu za ushindani.
Alishukuru kampuni ya Bantu kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya kuandaa filamu zenye ubora wa hali ya juu.
Kwa hisani ya Fullshangwe.
DR.MWAKYEMBE AWASHA MOTO TRL
Posted on June 14, 2012 by AmranBaada ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.
Licha ya kuagiza kutimuliwa kwa ofisa huyo, pia alitangaza kuandaliwa utaratibu wa kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha usafiri huo, ikiwamo kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 10 na pia kuondolewa kwa utaratibu wa malipo ya mizigo midogo ya abiria.Kusoma zaidi bofya Read more »
Ng’humbi amkatia rufaa Mnyika
Posted 0n June 14, 2012 by amranAliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng’umbi amewasilisha hati ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyompa ushindi John Mnyika.
Ngh’umbi, alifungua kesi dhidi ya Mnyika wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akipinga matokeo yaliyompa ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu kanuni na sheria ya uchaguzi katika uchaguzi huo .
Lakini Mahakama Kuu katika hukumu yake ilitupilia mbali madai na maombi ya Ngh’umbi na badala yake ikamthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo la Ubungo. Katika hukumu hiyo aliyoisoma Mei 24, 2012, Jaji Upendo Msuya alisema kuwa Ngh’umbi alishindwa kuthibitisha madai yake na kuonesha jinsi madai hayo yalivyoathiri matokeo ya uchaguzi huo.
Baada ya hukumu hiyo Ngh’umbi alielezea kutokuridhika na uamuzi huo na kudai kuwa anakwenda kujadiliana na wakili wake ili kuona ni hatua gani ya kuchukua. Jana Ngh’umbi kupitia kwa wakili wake, Issa Maige, alianza rasmi mchakato wa kupinga hukumu hiyo baada ya aliwasilisha Mahakama ya Rufani hati ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
CHANZO:MWANANCHI

No comments:
Post a Comment