amreezle

amreezle

Wednesday, April 25, 2012

Amran

Kibaki asema serikali haitakubali kujitenga kwa jimbo la Pwani

Posted on April 25, 2012 by amran

Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imetoa onyo kwa makundi yanayopigania kujitenga kwa jimbo la pwani kutoka taifa la Kenya akihutubia kikao cha bunge mjini Nairobi kwa mara ya kwanza tangu kuidhinishwa katiba mpya rais Mwai Kibaki amesema serikali haitakubali kujitenga kwa jimbo la Pwani kutoka taifa la Kenya.
Kwa mujibu wa VOA rais huyo amesema jimbo la Pwani ni ardhi ya Kenya na jimbo hilo halitakubaliwa kujitenga. amesema Kenya ni taifa moja juhudi zozote za kulihgawanya taifa hilo zitakataliwa.Kusoma zaidi bofya Read more »

Lipumba: JK amemziba Pinda mdomo

Posted on April 25, 2012 by amran
Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka jamii kutomhukumu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kushindwa kushughulikia madai ya wabunge kutaka mawaziri wajiuzulu akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete amemziba mdomo.
Kwa mujibu wa Mwananchi akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema hata kama Pinda angekuwa na utashi wa kuzungumzia suala hilo, asingeweza kusema chochote kwa kuwa Rais Kikwete alimziba mdomo… “na suala hilo pia liko juu yake.” Kusoma zaidi bofya Read more »

Mzee atuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12!

Posted on April 25, 2012 by amran
Huku tukiendelea kupambana na ufisadi jamii yetu bado ina kazi kubwa kwa masuala mengine kama vile ubakaji ungana na Habari leo wakiripoti balaa hili.
Polisi katika Mkoa wa Kusini, inatarajia kumfikisha katika Mahakama ya Mwera Wilaya ya Kati Unguja, mkazi wa kijiji cha Machui, Suleiman Khamis Mihayo (67) kujibu mashitaka ya kumbaka msichana wa miaka 12 (jina tunalihifadhi) katika eneo la Machuwi Wilaya ya Kati Unguja.
Mkuu wa Dawati la Watoto katika kituo cha Polisi cha Mwera, ACP Khadija Haji Khatib alisema Mihayo aliripotiwa wiki iliyopita baada ya mtoto huyo kutuhumiwa kuiba mali za Mihayo ambazo ni nguo pamoja na nazi.
Hata hivyo, mtoto huyo baada ya kuhojiwa na polisi, inadaiwa alimtuhumu Muhayo kufanya mapenzi naye kwa muda mrefu bila ya kumpa malipo ya fedha ndio maana akachukua mali hizo kujilipa ujira wake.Kusoma zaidi bofya Read more »

Hakimu ambembeleza Lulu mahakamani

Posted on April 24, 2012 
Mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu akilia wakati alipofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Picha na Michael Jamson.
Msanii wa filamu, Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akibubujikwa machozi kiasi cha kumfanya Hakimu Ritha Tarimo ambembeleze ili kumnyamazisha. Lulu anashtakiwa mahakamani hapo kwa kutuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba na alifikishwa jana kwa mara ya pili akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza na Polisi.
Kwa mujibu wa mwananchi Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 3:06 asubuhi akiwa katika basi dogo la Magereza pamoja na mahabusu wengine wanawake ambalo lilikuwa likisindikizwa na magari mengine mawili na alikuwa chini ya ulinzi wa askari sita wa kike wa Magereza na askari mmoja wa kike wa Polisi wakishirikiana na askari wa kiume wa Magereza zaidi ya sita. Kusoma zaidi bofya Read more »

Pinda aziba masikio mawaziri kujiuzulu -Ufisadi Maliasili unatisha

Posted in Uncategorized on April 24, 2012 by sunday Shomari
Wakati wabunge wakiendelea kusaini fomu ya majina ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni jana alikwepa kuzungumzia hatua za kinidhamu dhidi ya mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mwananchi akiahirisha Mkutano wa Saba bungeni Dodoma, Pinda hakugusia suala la kujiuzulu kwa mawaziri wanane na badala yake alisema: “Siku zote Serikali imekuwa tayari kupokea ushauri wa Bunge baada ya kusikiliza mjadala na mapendekezo ya waheshimiwa wabunge.’’
Baada ya kuahirishwa kwa Bunge hadi Juni 12, mwaka huu. Pinda akiwa nje ya Bunge alikwepa kuzungumzia suala hilo licha ya kubanwa na waandishi wa habari na badala yake alicheka: “Haahaa,” kisha akaingia kwenye gari na kuondoka. Kusoma zaidi bofya Read more »

No comments:

Post a Comment