Shambulizi la gruneti lauwa Nairobi!!
Posted on April 30, 2012Polisi nchini Kenya wanasema shambulizi la guruneti kwenye Kanisa moja jijini Nairobi limeuwa mtu mmoja Jumapili na kuwajeruhi vibaya wengine zaidi ya 10. Mpaka sasa hakuna aliyedai kufanya shambulizi hilo katika Kanisa hilo linalojulikana kama God’s House of Miracle International church lililoko katika mji mkuu wa Kenya.
Kwa mujibu wa VOA Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika siku 6 baada ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya kuonya juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi mjini Nairobi. Ubalozi huo ulitoa ujumbe huo ukionya raia wa Marekani kutahadhari.
Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na majengo mashuhuri ya serikali mjini Nairobi yakashambuliwa na magaidi. Aidha taarifa hiyo ya ubalozi ilisema wakati mahsusi wa shambulizi hilo hujulikani lakini yaaminika wanaopanga shambulizi hilo wamo katika hatua za mwisho.
JK KUBWAGA MAWAZIRI WENGI WA ZAMANI,SURA MPYA ZATABIRIWA
Posted on April 30, 2012Wakati mawaziri wanaounda Serikali ya Awamu ya Nne wakiendelea kupata usingizi wa mang’amung’amu kwa hofu ya kupanguliwa, kuna taarifa kwamba idadi kubwa ya mawaziri wa zamani wataachwa na sura mpya hususan vijana kutawala baraza jipya.
Kwa mujibu wa Mwananchi joto la mabadiliko ya Baraza la Mawaziri limeshika kasi baada ya Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam juzi na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa chama hicho, kuwataka mawaziri wanaoandamwa na kashfa mbalimbali katika wizara zao, kuachia ngazi.
Taarifa ya Rais Kikwete kutaka kusuka upya Baraza la Mawaziri ilitangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizikia kwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CCM.
Vyanzo vya Mwananchi vimeeleza kuwa mbali na Rais kutumia kigezo cha udhaifu uliobainishwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), atawaengua pia wale wanaoshindwa kuwajibika na wale wenye kasi ndogo ya uongozi. Kusoma zaidi bofya Read more »
No comments:
Post a Comment