SHUKRAN ZA RAIS WA JUMUIYA YA WATANZANIA
Posted in Uncategorized on April 19, 2012Nachukua fursa hii kuwashukuru rasmi kwa uchaguzi wa April 15 ambao umetupatia uongozi katika Jumuiya yetu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka mitano. Kwa hakika ushindi si kwa viongozi waliochaguliwa isipokuwa ni ushindi kwa Jumuiya yenyewe. Tulipo leo sio tulipokuwa April 14. Kwa pamoja tumeonyesha nia ya kuunganisha nguvu zetu rasmi na kuleta umoja ambao utasaidia katika maslahi yetu wote kijamii pamoja na taifa letu tunalolipenda– Tanzania.
Sisi mliotuchagua kuongoza juhudi hizo tuna jukumu la kuhakikisha tunatetea, kusikiliza na kuendeleza haki na maslahi ya kila mtanzania. Moyo tulioonyesha katika uchaguzi huu uendelee kuwa chachu ya kuhakikisha tunafanya kazi kwa pamoja, kuinua Jumuiya yetu mpaka pale ambapo tunadhani inastahili kuwepo.
Kama tulikwaruzana katika mchakato huu basi tusameheane, tusirudie makosa na tuangalie mbele kama Jumuiya yenye umoja, upendo na ustahimilivu.
Maana halisi ya Demokrasia iliyokomaa ni kwamba baada ya uchaguzi kwisha Kazi na kipindi muhimu cha kufanya kazi kwa pamoja kinaanza.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Jumuiya DMV
Wenu ,
Rais,
Iddi Sandaly.
KWAHERI DISCOVERY
Posted in Uncategorized on April 19, 2012SIMBA YAZIDI KUKARIBIA UBINGWA BARA
Posted in Uncategorized on April 19, 2012Mchezaji Uhuru Selemani wa timu ya Simba ya Tanzania kushoto akishangilia goli la kwanza alilofunga dhidi ya timu ya JKT Ruvu pamoja na na wachezaji wenzake Gervas Kago kulia na Patrick Mafisango, Simba imecheza na JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo Simba imeshinda magoli 3-0 yakifungwa na wachezaji Uhuru Selemani mwenyewe,Haruna Moshi “Boban”, na Mwinyi Kazimoto.Mchezo wa leo umeisogeza zaidi Simba kuelekea kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Vodacom Bara.(Kwa hisani ya Full Shangwe).
No comments:
Post a Comment