amreezle

amreezle

Monday, April 16, 2012

Mwenyekiti wa vijana CCM Arusha ajiengua

Posted in Uncategorized on April 17, 2012 

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha (UVCCM) James Ole Milya ametangaza kujiengua katika chama chake.
Kwa habari zaidi baadaye.

UMRI WA LULU

Posted in Uncategorized on April 17, 2012 

Utata wa umri wa Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi inayomhusisha na kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’ unazidi kugubika katika ishu hiyo baada ya baba yake mzazi, Michael Edward Kimemeta kuibuka na kutofautiana na watu wengine akiwemo mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila hivyo kushindwa kung’amua nani muongo na nani mkweli.
Kwa mujibu wa Global Publishers uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kuwa katika ishu hiyo, kuna mambo mengi yanayosemwa ya uongo na mengine ya ukweli. Kusoma zaidi bofya Read more »

WAZIRI NAHODHA MATATANI

Posted in Uncategorized on April 17, 2012 

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Shamsi Nahodha anachunguzwa , ni nadra sana kwa taarifa kama hizi kupatikana , Je waziri anaripotiwa kukwamisha baadhi ya mambo ni nini kitakacofanyika au kumkuta.
Ungana na Mwananchi kupata maelezo ya sakata hilo kwamba kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, inayoongozwa na Edward Lowassa imependekeza kuundwa kwa kamati teule ya watu wanne kumchunguza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha kwa madai ya kukataa kutekeleza agizo lake lililotaka nusu ya matrekta ya Kilimo Kwanza yaliyopelekwa Shirika la Uzalishaji Mali la Suma JKT, yapelekwe Magereza.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Lowassa alithibitisha kuundwa kwa kamati hiyo ndogo lakini akasema haina madaraka mpaka Spika, Anne Makinda, atakaporidhia.
“Ni kweli tumependekeza kuundwa kwa kamati ndogo kuchunguza jambo hilo na tumempelekea Spika, lakini kwa sasa haina madaraka yoyote mpaka Spika atakaporidhia kuundwa kwake na kuitangaza,” alisema Lowassa.
Spika wa Bunge Anne Makinda hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana mara kadhaa. Kusoma zaidi bofya Read more »

No comments:

Post a Comment