Makada CCM wamfuata James Millya Chadema
Posted on April 19, 2012Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Arusha kimezidi kutikisika baada ya viongozi wake kuendelea kujiondoa na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Siku mbili, baada ya Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James Ole Milya, kujiunga na Chadema, Diwani wa CCM, kata ya Sombetini mkoani humo, Alfonce Mawazo, naye amejiondoa na kujiunga na Chadema. Kusoma zaidi bofya Read more »
Zitto azilipua bungeni Tanesco, ATCL
Posted on April 19, 2012Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imependekeza kwa serikali iwakamate na kuwafikisha mahakamani maofisa wa serikali walioingia mkataba wa ukodishaji wa ndege ya ATCL, Air Bus 420-214, mwaka 2007.
Hali kadhalika, kamati hiyo imelishutumu Shirika la Umeme nchini (Tenesco), kwa kufanya manunuzi ya Sh. bilioni 600 bila kufuata sheria za manunuzi.
Kwa mujibu wa Nipashe hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, wakati akiwasilisha taarifa yake, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2010.Kusoma zaidi bofya Read more »
DR.MAGUFULI AUGUA GHAFLA NA KULAZWA YUKO ICU
Posted on April 19, 2012 by AmranWaziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa habari leo taarifa za kuugua kwa Waziri huyo zilitangazwa jana bungeni na Naibu Spika, Job Ndugai, wakati akiahirisha kikao cha Bunge mchana.
Ndugai alisema awali Magufuli alipelekwa hospitalini hapo akisumbuliwa na shinikizo la damu.
“Baada ya kufika hospitalini na kupatiwa matibabu alibainika kusumbuliwa na kichomi upande wa kushoto… bado amelazwa hospitalini na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikwenda kumwangalia,” alisema.
Pia Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), amenusurika kifo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, kupata ajali Morogoro. Kwa mujibu wa Ndugai, ajali hiyo ilitokea jumanne saa 12.15 asubuhi baada ya gari lake kugongwa na lori na kupinduka. Kusoma zaidi bofya Read more »
HONGERA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
Posted on April 19, 2012 by AmranDIDIER DROGBA AFANYA VITU VYAKE
Posted on April 19, 2012 by AMRANMshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba akishangilia bao lake pekee alilofunga dakika ya pili ya dakika za majeruhi baada ya kutimu dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London, England usiku huu katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya mabingwa watetezi, Barcelona ya Hispania. Chelsea sasa inahitaji sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano ugenini, Uwanja wa Camop Nou ili kutinga fainali, ambako itacheza na mshindi kati ya Bayern Munich ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania. Mechi ya kwanza jana mjini Munich, Real walifungwa 2-1 na wanahitaji ushindi japo wa 1-0 nyumbani, Santiago Bernabeu ili kutinga Fainali.
No comments:
Post a Comment