amreezle

amreezle

Saturday, April 28, 2012

JK aitisha Kamati Kuu CCM ghafla

Posted on April 28, 2012

Wakati joto la wabunge, vyama vya siasa na wanaharakati nchini kutaka mawaziri waliohusishwa na kashfa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wajiuzuluzu likizidi kupanda, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha ghafla cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya siasa nchini.
Habari zilizolifikia gazeti la Mwananchi na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, zilieleza kuwa kikao hicho kitafanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Ingawa Nape alisema hawezi kutaja ajenda za kikao hicho kwa kuwa ni siri, habari kutoka baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, zilidokeza kuwa hakuna namna, Rais Kikwete akakwepa kuzungumzia shinikizo la mawaziri hao kujiuzulu.Kusoma zaidi bofya Read more »
Posted on April 28, 2012 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amewajibu jeshi la polisi mkoani Mwanza kuwa, anawakaribisha wote wanaotangaza kutaka kumkamata kufuatia madai ya kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Mwananchi kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, kutangaza kumchukulia hatua za kisheria Katibu Mkuu huyo.
Akiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Sahara, Dk Slaa alitoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuwakamata wale wote waliohusika na vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.Kusoma zaidi bofya Read more »

No comments:

Post a Comment