WAZIRI MKULO NJIA PANDA SASA!
Mapambano na ufisadi ni changamoto katika serikali ya rais Jakaya Kikwete hivi sasa kashfa zimeelekea katika wizara ya fedha na waziri mhusika ana kazi ya kueleza fuatana na gazeti la Mwananchi kuhusiana na hilo.
kashfa ya uuzwaji wa kiwanja cha Serikali namba 10 kilichoko Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL), imemuweka njiapanda Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho, uliihusisha wizara yake na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mkulo aliwahi kuingia kwenye mvutano na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe baada ya kuituhumu kamati hiyo kuhongwa ili kutetea nyongeza ya muda ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC). Kusoma zaidi bofya Read more »
UCHAGUZI DMV ULIKUWA WA KIHISTORIA!
Posted in Uncategorized on April 18, 2012/img_9667.jpg”>Hawa ndio wajumbe ya bodi.
Bw.Jacob Merere akipiga kura yake. Kwa picha zaidi bofya Read more »
Bw.Jacob Merere akipiga kura yake. Kwa picha zaidi bofya Read more »
Mama Kanumba atoa ya moyoni
Posted in Uncategorized on April 18, 2012 bMama mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba, amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (Shiwata) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae.
Kwa mujibu wa Nipashe akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na (Shiwata) jana jijini Dar es Salaam, Mama Kanumba, alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mtoto wake kila kona ya nchi.Kusoma zadi bofya Read more »
SHUKRANI ZA DHATI TOKA KWA LUVNESS
Posted in Uncategorized on April 18Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa Watanzania wote wa DMV kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huu wa uchaguzi kufika kwenu kwa wingi ndio kumefanya uchaguzi huu uwe wa kihistoria.
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote walioniunga mkono katika sera yangu ya MTANZANIA DMV BADILIKA ni jambo lakutia moyo kwa wanaDMV kusema kweli nimeguswa sana na moyo wenu wa upendo mliouonyesha kwangu, hasa timu yangu ya kampeni imefanya kazi ya ziada bila kujali muda wao.
Tatu nampongeza Iddi Seif Sandaly kwa kuchaguliwa dhidi yangu kuwa Rais wetu mpya wa Jumuiya yetu ya DMV popote pale panapo tokea mafahari wawili wanashindana lazima atokee mshindi na mshindwa kwa maana hiyo basi Ushindi wako Iddi Sandaly nimeupokea kwa mikono miwili na daima nitashiriana na wewe katika kusukuma gurudumu la maendelea DMV kama mwanajumuiya mwingine.
Mwisho, nakutakia kila la heri katika kazi yako mpya na naomba Watanzania wenzangu DMV tumuunge mkono Iddi Sandaly na uongozi wake ilikufanya kazi yao iwe rahisi. Asante na Mungu awabariki. MTANZANIA DMV BADILIKA.
No comments:
Post a Comment