amreezle

amreezle

Monday, April 23, 2012

Operesheni Uwajibikaji bungeni.

Postd on April 23, 2012
Mjumbe wa NEC CCM ndugu Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Musoma Vijijini amesaini waraka wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Serikali. Amekuwa Mbunge wa 74 kufanya hivyo na Mbunge wa 6 kutoka CCM. #OperesheniUwajibikaji-Zitto Kabwe-Fb.

PLOTS FOR SALE LOW DENSITY IN TANZANIA

Plots for sale at the following locations:
Mapinga Bagamoyo Road, 40m by 20m most plots 200 meters off Dar-Bagamoyo Rd.
Price-Tshs. 15 mill. approximately.
Also Njiro Hill Arusha near Tanzania Nuclear Regulatory Authority head office. Price Tshs 90 mill.

LINAH -LIVE IN BOSTON MASS..SAT MAY 12 “TAMANI USA TOUR” INAWASHA MOTO BALAAAAAAAA!!

Posted on April 23, 2012 

Je Pinda kumfuata Lowassa?

Posted on April 23, 2012

TIMU YA WATANZANIA DMV IMEKAMILISHA LENGO LAKE LA KUINGIA LIGI YA DIASPORA WOLD CUP 2012

Posted on April 23, 2012 
Na Ebou Shatry
Tanzania DMV imekamilisha madhumini na malengo ya kujiandaa rasmi na ligi ya Diaspora World Cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland, mwanzoni mwa mwenzi huu wa Mei chini ya mdhamini wa timu hiyo Abdallah wa Vizion One.
Taarifa kwa wachezaji wote mnaombwa kuzingatia muda wa mazoezi mliopangiwa ili kuwa makini na malengo yaliokusudiwa ya ligi ya Diaspora World cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland,
Pia katika bahati hii ya kushiriki kwenye ligi ya Diaspora World Cup, na kufanikisha malengo yaliokusudiwa, timu hiyo ya TZ DMV inawaomba Watanzania wote ushirikiano wenu wa kila hali ili kuipa changamoto timu ya Watanzania DMV pamoja na wachezaji, katika burudani inayopendwa na wengi ulimwenguni, karibuni karibuni sana siku ya sherehe za ufunguzi April 28th ndani ya Discovery Stadium uliopo Germantown SoccerPlex. Stadium.
Milango inatunguliwa saa sita mchana ambapo jamii zote zitawasili kuunga mkono time zao zilizoingia katika ligi hiyo kitaifa kama Diaspora World Cup pamoja na ngoma za kiasili, nyote mnakaribishwa.
Vile vile vigogo wengi wamethibitisha uwepo wao ikiwa ni pamoja na HE Eklil Hakimi, Mheshimiwa Balozi wa Afghanistan katika Umoja wa Mataifa, HE Joseph Foe-Atangana, Mheshimiwa Balozi wa Cameroon katika Umoja wa Mataifa, HE Perezi K. Kamunanwire, Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Marekani, HE Adebowale mimi. Adefuye, Mheshimiwa Balozi wa Nigeria nchini Marekani, HE Devinda R. Subasinghe, aliyekuwa Balozi wa Sri Lanka, Waziri Johnny Moloto, Mkuu wa Mission wa Afrika Kusini nchini Marekani, Jenerali Emmanuel Maganga, wa Tanzania katika Ubalozi wa Marekani, na kamanda Luther Reynolds, Mkuu wa Polisi wa Germantown atakuwepo,
Adress MD. 14501 Schaeffer Rd
Germantown, MD20874

Watu kadhaa watiwa mbaroni Zanzibar

Posted on April 23, 2012

Jeshi la polisi Zanzibar limewatia mbaroni watu zaidi ya 12 kwa madai ya kukataa kutii amri ya jeshi hilo ya kutakiwa kuondoka katika viwanja vya baraza la wawakilishi, walipokwenda kuonana na Spika na Baraza hilo Pandu Ameir Kificho.

CHANZO:Mzalendo.net

Stock Market Newsletter

Posted on April 22, 2012
David Magness
JAPAN has now SHUT DOWN 53 of its 54 Nuclear Reactors…since the Fukushima Daiichi Reactor was damaged by a Tsunami and Earthquake March 11, 2011…and has returned to fossil fuels…and all building of nuclear reactors has stopped in Japan…
…This is causing the Japanese economic recovery to SLOW DOWN…and will cause parts of Southeast Asia to be affected…
…At the moment…ONLY CHINA is building Nuclear reactors…at a rate of one per week…These are small reactors…used for communities of 20,000 residents or less…The COMMUNIST PARTY is afraid of a CIVIL WAR by the 80% “HAVE NOTS”…who have been neglected by THE PARTY for the past 60 years…since CHINA became “RED”… in OCTOBER 1949…
…Many of these communities still don’t have electric light…so the SAFETY of the new reactors IS IN QUESTION…as the Communist Party rushes to CATCH UP…
…Technically…the market LAST WEEK Avoided a “SELL SIGNAL” by ONLY days…USING the old TURTLE TRADING SIGNAL…that says IF after a MARKET TOP…IF the market CLOSES below the LOW of the PAST 20 days…the MARKET RALLY would BE OVER…
…IT DIDN’T…so this newsletter comes to you ONE WEEK LATE…with the “RALLY INTACT”…but STILL waiting for this to “Play Out”…
…SUMMARY…Using W.D. GANN’s formula…we have a SERIOUS MARKET DATE coming up…May 15th…IF we get past THIS DATE…the NEXT BUMPER will be JUNE 11-15th…At that POINT…we believe the Springtime Rally will FINALLY be over UNTIL FALL…Until…OCTOBER…ONE MONTH BEFORE the Elections…
…TSP Participants should MOVE to the C FUND…[S&P 500]…

Sarkozy ashindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi

Posted on April 22, 2012

Mgombea kiti cha rais wa chama cha Socialist, Francois Hollande amepata ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Ufaransa Jumapili, akijipatia asili mia 29.3 za kura. Mpinzani wake kiongozi wa vyama vya kihafidhina rais Nicplas Sarkozy amepata asili mia 26 za kura.
Kwa mujibun wa VOA wanasiasa hao wawili watapambana katika duru ya pili hapo Mei 6. Matokeo hayo yalitarajiwa kutokana na uchunguzi kadha wa maoni uliofanywa kabla ya uchaguzi wa Jumapili ukionyesha kwamba Hollande atamshinda Sarkozy katika duru ya kwanza na ya pili. Kusoma zaidi bofya Read more »

Ridhiwani Kikwete amshukia Millya

Posted on April 22, 2012 

Baada ya kujiengua UVCCCM Mwenyekiti wa Umoja huo mkoani Arusha amepokea dozi ya vijembe kutoka viongozi mbali mbali wa Umoja huo pamoja na CCM.
Ungana na Nipashe upate yale aliyotoa Ridhwani Kikwete kwa kiongozi huyo wa zamani wa UVCCM
Mtoto wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha, James Ole Millya.
Millya alijiengua kutoka CCM na kujiunga CHADEMA kutokana na kile alichoeleza kuwa chama tawala kimekuwa mfano wa gari lililosheni pancha, hivyo halifai kwa safari.
Hata hivyo, baada ya Millya kuondoka CCM, taarifa zilizopatikana mkoani humo zilieleza kwamba aliondoka akiwa na takribani Shilingi milioni 2, mali ya UVCCM.
Taarifa hizo ndizo zimemuibua Ridhiwani akichangia katika mtandao wa kijamii wa Tunuru la Afrika na kusema Millya asubiri utaratibu unafuata. Kusoma zaidi bofya Read more »

BANDARI YA DAR YAIBUA MAPYA-Wabunge wahoji iweje serikali itegemee upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni

Posted 0n April 22, 2012 Ujenzi wa gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam Jumamosi ulizua tafrani bungeni kutokana na mabishano makali baina ya Kamati ya Miundombinu inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na baadhi ya wabunge.
Mabishano hayo yalitokea kuhusu upembuzi yakinifu unaodaiwa kufanywa na kampuni ya kigeni China Communication Construon Company (CCC), kuhusu ujenzi wa gati hizo na kuweka ghalama ya dola za Marekani milioni 325.
Wabunge wengi walihoji iweje serikali itegemee upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni ambayo wakati huo huo ndiyo inatarajiwa kupewa zabuni ya kujenga gati hizo.
Mbunge wa Ubungo, Chadema John Mnyika, alitaka serikali iteue kampuni inayojitegemea kwa ajili yaa kufanya upya upembuzi yakinifu ili kujua gharama halisi zitakazotumika kujenga gati hizo.
Alisema kutegemea upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya kigeni kunaweza kulitia hasara kubwa taifa hivyo alitahadharisha serikali ijiridhishe kwanza kabla ya kutoa zabuni ya ujenzi.
Awali, katika ripoti ya Kamati ya Miundombinu, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Peter Serukamba, ilisema Mamlaka ya Bandari TPA ikishirikiana na kampuni hiyo ya China, ilishafanya upembuzi yakinifu hivyo hakuna haja ya kurudia upya.
Serukamba alisema kuanza upya kufanya upembuzi yakinifu ni kupoteza muda wa ujenzi wa gati hizo ambazo zilianza kuzungumzwa tangu mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment