NIMESHINDWA UBUNGE WA EAC SASA KUJIPANGA UPYA -WILLIAM MALECELA
Posted in Uncategorized on April 18, 2012 by sunday ShomariWell, Heshima mbele sana JF KUMKOMA NYANI, leo kwenye uchaguzi wa Ubunge wa EAC nimeshindwa fairly na sina malalamiko, ninawapa hongera washindi wote walioshinda leo na hasa my best Friends Shyrose, Dulla, na Makongoro, MUNGU AWAONGEZEE NA WAKATUMIKIE VYEMA TAIFA LETU!
AS FOR ME SASA NI WAKATI WA KUKAA CHINI NA KUTAFAKARI NILIPOKOSEAA NA KUANZA KUJIPANGA UPYA, NINAWASHUKURU BAADHI YA JFs WALIONISAIDIA KWA HALI NA MALI, MBARIKIWE!
WAKUU WANGU MWANAKIJIJI, INVISIBLE NA HALISI, SINA CHA KUWALIPA KWA ALL YOU DID KATIKA KUNISAIDIA NA KAMPENI, WOTE MBARIKIWE NA MUNGU WA MBINGUNI NA JF WOTE MBARIKIWE, THIS IS MY HOME SO TUNAENDELEA KAMA KAWAIDA!
MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA AIBARIKI JF!”
William @Dodoma City!- Chanzo- jamiiforums.com
Makongoro,Kimbisa,Shy-Rose juu
Posted in Uncategorized on April 18, 2012 by sunday ShomariBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana liliwachagua Watanzania tisa kuingia katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma.
Katika uchaguzi huo, Twaha Taslima wa Cuf na Nderakindo Kessy wa NCCR-Mageuzi walichaguliwa kwa upande wa vyama vya upinzani. Taslima alipata kura 175 na Kessy kura 113.
Kabla ya uchaguzi wa jana, upinzani ulikuwa na nafasi moja katika bunge hilo ambayo ilikuwa inashikiliwa na Dk Fortunatus Masha wa UDP ambaye alianguka baada ya kupata kura 58.
Kwa upande wa wagombea wa CCM, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Charles Makongoro Nyerere, Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Shy-Rose Bhanji na Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Adam Kimbisa walishinda.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema Bhanji alishika nafasi ya pili katika kundi la kwanza (wanawake) akipata kura 120 akitanguliwa na Angela Kizigha aliyepata kura 166. Wote ni kutoka CCM.
Wengine waliogombea katika kundi hilo ni Rose Mwalusamba wa CUF ambaye licha ya kujitoa alipata kura saba, Fancy Haji Nkuhi (57), Dk Goodbertha Kinyondo (32), Janet Mmari (119) na Janet Mbene (87).
Katika kundi la pili kutoka Zanzibar, Abdullah Ali Hassan Mwinyi alirejea tena katika bunge hilo baada ya kuongoza kwa kupata kura 227 akifuatiwa na Mariam Ussi Yahya (91).
Katika kundi hilo, Septuu Nassor Mohammed na Dk Said Gharib Billal () walishindwa kurejea katika bunge hilo baada ya kuambulia kura 74 na 88 mtawalia. Wengine walioshindwa ni Dk Ahmada Hamid Khatibu (36), Dk Haji Mwita Haji (11), Khamisi Jabir Makame (6) na Zubeir Ali Maulid (39).
Katika kundi la vyama vya upinzani, mbali ya Dk Masha wengine walioshindwa ni Anthony Komu wa Chadema (93), Juju Danda wa NCCR-Mageuzi (23), Micah Mrindoko wa TLP (66) na Mwaiseje Polisya wa NCCR-Mageuzi (42).
Katika kundi la nne la Tanzania Bara, Kimbisa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam aliongoza kwa kupata kura 210 akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bernard Murunya aliyepata kura 135 na Makongoro kura 123.
Walioshindwa katika kundi hilo ni Dk Edmund Mndolwa (42), Elibariki Kingu (31), Dk Evans Rwaikiza (78), Mrisho Gambo (75) na Siraju Kaboyonga (38) wote kutoka CCM na John Lifa Chipaka wa Tadea (8).
CHANZO :MWANANCHI.
KHARTOUM YATANGAZA UYADUI NA KUSINI.
Posted in Uncategorized on April 18, 2012 by sunday ShomariBunge la Sudan limetangaza kuwa Sudan Kusini ni adui kati kati ya ghasia zinazosambaa kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa VOA baada ya upigaji kura mjini Khartoum jumatatu, waziri wa habari wa Sudan Kusini Barnaba Marial aliupinga uamuzi huo na kusema nchi yake si adui wa Sudan.
Rabi Abdelati Obeid mwanachama maarufu wa chama kinachotawala Sudan cha National Congress aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hali kati ya nchi hizo mbili hivi sasa ni hali ya kivita.
Alisema Sudan Kusini haiheshimu mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini.
RUSHWA NJE NJE UBUNGE AFRIKA MASHARIKI
Posted in Uncategorized on April 18, 2012 Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (kulia) akimwinamia Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wakati akimwomba ampigie kura iliaweze kuchukuwa nafasi hiyo kwa wagombea kutoka Tanzania Bara, Bungeni mjini Dodoma jana. (Picha na Edwin Mjwahuzi).
Je rushwa na ufisadi vimehalalishwa kwenye masuala ya kampeni ungana na Mwananchi kuona jinsi suala hilo lilivyo katika kampeni za ubunge wa Afrika Mashariki.
Kampeni za lala salama za kuwania nafasi za Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) mjini hapa, zinadaiwa kugubikwa na rushwa kwa baadhi ya wabunge wakidaiwa kupewa kati ya Sh100,000 na Sh milioni moja.Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kwamba mbunge mmoja amekabidhiwa kitita cha Sh5 milioni ili kuzigawa kwa baadhi ya wabunge.
Baadhi ya wabunge na wagombea waliohojiwa jana, walithibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo vya rushwa huku wakishangaa ukimya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Kusoma zaidi bofya Read more »
Je rushwa na ufisadi vimehalalishwa kwenye masuala ya kampeni ungana na Mwananchi kuona jinsi suala hilo lilivyo katika kampeni za ubunge wa Afrika Mashariki.
Kampeni za lala salama za kuwania nafasi za Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) mjini hapa, zinadaiwa kugubikwa na rushwa kwa baadhi ya wabunge wakidaiwa kupewa kati ya Sh100,000 na Sh milioni moja.Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kwamba mbunge mmoja amekabidhiwa kitita cha Sh5 milioni ili kuzigawa kwa baadhi ya wabunge.
Baadhi ya wabunge na wagombea waliohojiwa jana, walithibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo vya rushwa huku wakishangaa ukimya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Kusoma zaidi bofya Read more »
No comments:
Post a Comment