amreezle

amreezle

Thursday, April 19, 2012

KITENDAWILI CHA UFISADI TANZANIA BADO NGUMU – Ufisadi wa mabilioni kila kona

Posted on April 20, 2012

Ufisadi , ufisadi , ufisadi uwajibikaji utakuja lini hii ni wazi kama nilivyosema awali kazi ya mapambano 5Tanzania bado ni kubwa! fuatana na gazeti la Mwananchi kwa ripoti ifuatayo Wabunge Jumanne waliijia juu Serikali kwa matumizi mabaya ya fedha za umma na ufisadi ulijitokeza kwenye taasisi zake mbalimbali katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, mwaka jana.
Hasira za wabunge hao zilitokana na ripoti tatu za Kamati za Bunge; Mashirika ya Umma (POAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Serikali Kuu (PAC) kuonyesha upotevu wa mabilioni ya shilingi yaliyotumika katika nyanja mbalimbali ikiwemo mishahara hewa na mikataba mibovu.
Mbunge wa Longido (CCM), Michael Laizer alisema ni aibu kila mwaka kuwa na ripoti za wizi wa mali za umma lakini Serikali inakaa kimya. Kusoma zaidi bofya Read more »

KIBAO CHA LEO KUTOKA KENYA -SIRI YA PENZI

Posted on April 20, 2012 

Kimbunga cha Ole Millya chazidi kuifagia CCM

Posted in Uncategorized on April 20, 2012 by sunday Shomari

Kasi ya wanachama wa CCM kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema mkoani Arusha imezidi kuongezeka baada ya wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wilayani Ngorongoro kukihama chama hicho jana.
Kwa mujibu wa Mwananchi mbali na viongozi hao, pia Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga na Diwani wa Kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema, mkoani Mwanza Hamis Mwagoa, jana walitangaza kuhamia Chadema.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema atachukua rasmi kadi ya Chadema kesho akiwa na wenzake kadhaa ambao hakutaka kuwataja.Kusoma zaidi bofya Read more »

NIMR IMEGUNFUA KIFAA KIPYA CHA KUPIMA KIFUA KIKUU

Posted on April 20, 2012 
Dr.-Mwele-Ntuli-Malecela.
Taasisi ya taifa ya utafiti ya magonjwa ya binadamu (NIMR) imegundua kifaa kipya kijulikanacho kama Genexpert kwa ajili kupima ugonjwa wa kifua kikuu(TB)
Akizungumza katika mkutano wa 26 wa taasisi ya tafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR)mratibu wa tafiti za kifua kikuu katika kituo cha NIMR Mbeya Dkt.Elias Nyanda alisema kuwa kifaa hicho kimethibitishwa na shirika la afya ulimwenguni(WHO).
Alisema kuwa kifaa hicho cha kisasa kina gundua vimelea vya kifua kikuu vyenye vina saba ambavyo vinagundua wadudu walioko kwenye ugonjwa wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili na mgonjwa akapata majibu yake.
Aidha alisema kuwa faida ya kifaa hiki cha kisasa ni pamoja na kugundua kifua kikuu na usugu wa dawa ambapo kifaa kilichokuwa kinatumika awali cha darubini hakikuwa na uwezo huo.
Faida nyingine ni kupunguza uwezo wa kuambukiza ugonjwa huo ambapo hapo awali wagonjwa wa kifua kikuu walioonekana kuwa na ugonjwa huo lakini baada ya kupimwa wakaonekana hawana kwa asilimia 60.
“Kifaa hiki kinagundua kwa haraka sana usugu mwingi ambao mgonjwa amekaa nao kwani mtu akiachwa bila kutibiwa ni wazi kuwa atasambaza mapema kwa watu wengine”alisema Nyanda.
Hata hivyo alitaja changamoto zinazowakabili kutokana na kifaa hicho kuwa ni pamoja na gharama kubwa sana lakini watengenezaji na mashirika ya kifedha wanaja
ribu kupunguza bei kwa nchi zinazoendelea ili kila nchi iweze kuwa na kifaa hicho.
Mbali na hayo alisema kuwa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa mkoa unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa asilimia nyingi wa wagonjwa ndiko wanapotokea.
CHANZO:FULLSHANGWE

SPIKA WA BUNGE TANZANIA AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI

Posted on April 20, 2012

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pomoja na katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kumaliza mazungumzo naye Ofisini kwake Dodoma alhamisi. Balozi Sefua alimtembelea Spika wa Bunge Ofisi kwake mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Sudan na Sudan kusini zaonywa juu ya kurudi vitani

Posted on April 19, 2012

Mkuu wa Umoja wa mataifa amesema Sudan Kusini kulikalia kimabavu eneo la uzalishaji mafuta la Heglig ni kinyume cha sheria na kukiuka utaifa wa nchi jirani ya Sudan.
Kwa mujibu wa VOA akiongea na waandishi wa habari mjini New York alhamisi katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliwaomba Sudan Kusini kuondoa majeshi yao kwenye eneo hilo la mpakani lenye utajiri wa mafuta ambalo linadaiwa na nchi zote mbili.
Bw.Ban pia aliitaka Sudan kuacha kufanya mashambulizi na kupiga mabomu maeneo ya Sudan Kusini na kuondoka kutoka kwenye eneo lenye mzozo la Abyei.

No comments:

Post a Comment