....MCHUNGAJI ALIETABIRI KIAMA....AIBUKA TENA!
Mchungaji toka California,Harold Camping mwenye umri wa miaka 89 amejitokeza toka machimboni na kutangaza kwenye radio yake ya Family Radio kuwa walikosea mahesabu ya biblia wakati wa kutabiri mwisho wa dunia,lakini Oktoba 21 mwaka huu kiama aka Judgment day kitatokea kweli na kuua watu wote ambapo watu wema watapaishwa mbinguni kuonana na Yesu Mchungaji huyo wa California alisema kuwa kutotokea kwa kiama May 21 kumetokana sana na nguvu za kiroho na wala si nguvu za asili,na kuongeza kuwa Mungu aliwaonea huruma watu kuwaangamiza kwa matetemeko makubwa ya ardhi lakini hiyo Oktoba 21 hakutakuwa na huruma ya Mungu na kiama kitatokea kweli na dunia itaangamizwa na itatoweka ndani ya muda mchache
No comments:
Post a Comment