LIL WAYNE....ALBUM YA MWISHO....KUSTAAFU GAME..?!
Young Money CEO,Dwayne Michael Carter Jr. aka Lil Wayne amefunguka huenda album yake ya The Carter IV ikawa nia ya mwisho na amepanga kustaafu game akiwa na miaka 35
....YOUNG MONEY ARTISTS....
Weezy kwa sasa ana miaka 29 coz amezaliwa September 27,1982 na amefunguka sababu kadhaa zikiwemo kuwa,amekua kwenye game kwa miaka 18 sasa na amekamilisha karibu yote anayoyahitaji,Pamoja kuwa na label ya Young Money na kufanikiwa kuwatoa Artist Nick Minaj na Drake na kwa baada ya mafanikio hayo yote,angependa baada ya miaka 6 ijayo (akiwa na miaka 35) awe amepumzika na familia yake....akila bata tu
MSANII MYCO CHRIS....AWEKA HISTORIA UGANDA...!
Msanii toka Uganda,Myco Chris ameweka historia ya kuwa Msanii wa kwanza toka Uganda kushinda tuzo ya kimataifa baada ya kupata tuzo ya best male UK Based Afro/Caribbean Act Black Entertainment Film Fashion Television And Arts (BEFFTA 2011)
Kwenye tuzo hizo kulikua na artist wenye majina makubwa waliogonga show,lakini Myco alipiga bonge la show na ngoma yake aliyofanya collabo na Kuklee ilipata shangwe za kutosha na kupewa heshima ya the man of the night
KARDINAL OFFISHALL....AKIMBIA AL-SHABAB....KENYA...!
Canadian Hip Hop Artist,Jason Harrow aka Kardinal Offishall ametua nchini Kenya akifuatana na shirika la World Vision Canada pande za Moyale na Garbatullah
....KARDINAL OFFISHALL PANDE ZA KENYA....
Kardinal na manager wake MayDay walitarajiwa kutembelea kambi ya wakimbizi ya Dadaab lakini baada ya watoa misaada 2 toka hispania kukamatwa na kundi la Al Shabaab ilibidi wasiende tena na alionekana pande za Nairobi hotel na huenda mambo yakitulia atarudi tena nchini Kenya kwenye project hiyo
THE DREAM,CHRISTINA MILIAN....WAMWAGANA RASMI...!
Baada ya kupita zaidi ya mwaka ya kuripotiwa kupeana talaka kutemana Celebz Atrist,Terius Youngdell Nash aka The Dream na recording artist,actress,dancer na model,Christine Marié Flores aka Christina Milian kwa sasa wametengana rasmi
....SIKU YA HARUSI....
Jaji wa Mahakama ya Fulton County,Ga. alimaliza utata wa makaratasi ya talaka yaliwasilishwa pande hizo,na kufunguka kuwa kwa sasa kila mtu yuko single na kuivunja rasmi ndoa ya the dream na Christina Milian iliyofungwa jijini Las Vegas,September 2009.Na mwezi July 2010,The-Dream alifunguka kuwa yeye na Christina Milian walitengana miezi 3 tu baada ya ndoa yao..!
ARTIST AZIZ AZION....AMSHITAKI PROMOTER...UGANDA!
AZIZ AZION - UGANDAN ARTIST Artist Aziz Azion toka Uganda amefungua kesi kwenye mahakama ya Mengo dhidi ya promoter anayekwenda kwa jina la Kisseka Irene kwa kushindwa kumlipa deni lake la milioni 8 za Uganda anazomdai
Deni hilo linatokana na concert iliyoandaliwa na Kisseka pande za Kavumba Recreation Center mwezi May mwaka jana na kuelewana kupiga mzigo kwa Shs milioni 12 na Aziz Azioin kulipwa advance ya Shs milioni 4 tu na milioni 8angemaliziwa baadaye....Lakini hadi leo....Hakunaga
TENA....1 AUWAWA,15 WAJERUHIWA....NAIROBI-KENYA!
Kumetoa mlipuko mwingine jijini Nairobi,Jumatatu usiku kwenye Pub pande Mfangano Street na kuua mtu 1 na wengi 15 wamejeruhiwa na kupelekwa Kenyatta National Hospital (KNH) kwa matibabu zaidi,ikiwa ni masaa 24 tu baada ya mlipuko wa kwanza uliotokea Jumapili usiku na kujeruhi zaidi ya watu 14
....MAJERUHI PANDE ZA KENYATTA NAIROBI HOSPITAL....
Kati ya watu hao 15 waliojeruhiwa,2 kati yao wana hali mbaya na mashuhuda walisema kuwa mlipuko huo ulitokea saa 2 usiku,wakati raia wakipanda matatu kurejea majumbani na baada ya kutokea mlipuko huo mkubwa wengi walidhani ni pancha lakini kumbe lilikua ni bomu la kutupa mkono
CHRIS BROWN vs RIHANNA...KUWANIA TUZO MOJA..!
Artist waliokua wana-share malavidavi Rihanna na Chris Brown wamechaguliwa kugombea category moja kwenye tuzo za Soul Train Awards 2011
Rihana na Chris Brown wanagombania tuzo ya The Best Dance Performance na Rihanna anagombea kupitia track yake ya Only Girl (In The World)/What’s My Name,wakati Chris Brown ameingia na track yake ya She Ain’t You na kufanya awe anagombea category 5 tofauti ikiwemo Song Of The Year na Album Of The Year wakati Artist Beyoncé Knowles aka Mrs Jigga anawania tuzo 4 na tuzo hizo zitatolewa jijini Atlanta-Marekani,tarehe 17 November,2011
....BOMU LAJERUHI WATU CLUB....NCHINI KENYA...!
Watu zaidi ya 13 wamejeruhiwa jijini Nairobi-Kenya na kukimbizwa Kenyatta Hospital baada ya bomu la kutupwa na mkono aka grenade kurushwa kwenye nightclub iitwayo Mwauras club leo asubuhi
Shuhuda wa tukio hilo,alifunguka kuwa kuna jamaa alikuja pande za Mwauras bar saa 9 za usiku na kuomba kuingia ndani na kurusha bomu hilo na kukimbia na polisi wa Kenya hawajufunguka ni nani muhusika,lakini kundi la waasi wa Al-Shabab toka somalia linahusishwa na tukio hilo hasa baada ya Majeshi ya Kenya kuamua kuwasaka kundi la Al-Shabab baada ya kufanya tukio la utekaji nyara wa mtalii toka Uingereza,mmoja toka Ufaransa ambaye baadaye alifariki na wafanyakazi 2 wa misaada toka Hispania waliofika Kenya na wiki iliyopita Ubalozi wa Marekani uliwatahadharisha wakenya kuwa makini na mashambulio kama hayo toka kwa kundi la Al-Shabab
.....ETI DIAMOND NA WEMA....WARUDIANA TENA....?!
Sarakasi za 'Love-Cartoon' kali star wa Bongo Flava,Naseeb Abdul aka Diamond baada ya kutangaza kummwaga Wema Sepetu (Miss TZ 2006-2007) kwa sasa zimefunguliwa upya kuwa busara za mama mzazi wa Diamond,Sanura Khassim ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike....
....MOYO WANGU....
Imefunguliwa kuwa baada ya Wema kupiga simu na 'kulia lia' kwa mkwe kuwa atakunywa sumu,Mama Mkwe aliwaita Wema na Diamond na wajomba zake nyumbani kwake,ili wazungumze na baada ya mvutano wa muda mrefu,wajomba na Mama walikomaa Diamond alinywea akasalimu amri mbele ya wakubwa na kurudiana na lovi-davi wake aliye-make sana headlines kwa kutoka na Ma-Star wa bongo kuanzia....Steven Kanumba, Charles Baba,Hartmann Mbilinyi na Jumbe Yusuf
NICOLE,LEWIS HAMILTON....WAMWAGANA....!
Uhusiano wa kimalavidavi kati ya Celebs Artist toka kundi la Pussycat Dolls,Nicole Scherzinger na Dereva Lewis Hamilton toka Uingereza....umeisha
....ENZI HIZO....
Nicole na Hamilton walikua na uhusiano wa miaka 4,na wameachana baada ya kushindwa kuelewana mambo kadhaa coz walikua wanaishi nchi tofauti,Nicole anaishi Marekani na Lewis nchini Uingereza na uhusiano wao ulikua na wakati mgumu sana
JASON DERULO....JORDIN SPARKS....DAM DAM...!
JASON DERULO - R & B ARTIST
R & B stars toka Marekani,Jason Derulo na Jordin Sparks kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimalavidavi baada ya kuonekana wakiwa 'benet' sana hivi karibuni
JORDIN SPARKS - R & B ARTIST
Jordin Sparks alionekana kwneye birthdate ya Jason Derulo,alipotimiza miaka 22 na kuonezeka kwenye list ya Artist wenye mahusiano,kuanzia Jay Z vs Bewyonce,Alicia Keys vs Swizz Beatz na wengine wengi japo kutokana na uzoefu mara nyingi mahusiano ya watu maarufu huwa hayadumu,mfano Chris Brown na Rihanna na wengineo....
No comments:
Post a Comment