amreezle

amreezle

Saturday, October 8, 2011

daima atakumbukwa!

Steve 'the briliance' Jobs, alikuwa sehemu muhimu ya ubongo wa Apple katika uvumbuzi wa iPhone
Steve Jobs, ambaye anatambulika kama mvumbuzi wa vifaa vya kisasa zaidi vya mawasiliano vya iPhone, amefariki dunia.
Jobs, ambaye anaelezwa kuwa injini ya mabadiliko makubwa zaidi ya kiteknolojia duniani kupitia kampuni ya Apple, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 56, kwa mujibu wa msemaji wa kampuni hiyo inayoongoza kwa ubora wa bidhaa za kiteknolojia hivi sasa.
“Ubunifu, ustahamilivu na kujitoa kwa Steve, vilikuwa chanzo cha mabadiliko yasiyoweza kuelezeka kwa maneno katika kampuni ya Apple” ilisema sehemu ya taarifa ya Apple kuhusu kifo cha mtaalamu huyo.
Amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ambao alitangaza rasmi kuwa unamsumbua mnamo mwaka 2004, na licha ya jitihada za kukabiliana nayo kwa muda mrefu, ilishindikana kiasi cha mwaka 2008, kulazimika kuachia ngazi kama mtendaji mkuu wa Apple, huku akiwa ameshaiweka kampuni hiyo katika matawi ya juu sana kiteknolojia na katika ushindani wa soko.
Na miongoni mwa watu ambao wameonyesha wazi wazi kuguswa na msiba wa gwiji huyo wa teknolojia Marekani, ni pamoja na rais wa Marekani, Barack Obama, pamoja na tajiri wa kampuni shindani ya Apple, ya Microsoft, ndugu Bill Gates, ambao wote kwa pamoja wamesema kuwa kifo cha Jobs, ni pigo kubwa sio tu kwa familia yake bali kwa ulimwengu mzima ulionufaika na uvumbuzi wake wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment