amreezle

amreezle

Saturday, October 8, 2011

Kutoka pande za Mwanza ndani ya Tetemesha Records kuna kijana ambaye bila hiana wala kwere,twaweza sema anafanya vizuri katika medani za muziki wa kizazi kipya.Anaitwa Sagna(pichani).Ana wimbo mpya unaokwenda kwa jina “Yamenishinda” ukiwa ni mwendelezo wa wimbo wake “Mganga”.
Je, ni kweli kwamba kuna dawa ya mapenzi?Ni kweli kwamba “karumanzira” anaweza kusababisha mshawasha wa mahaba ndani ya nyumba ukazidi? Kuna ukweli wowote kwamba “mzee wa busara” anaweza kusababisha fulani atoke kwa yule wake na aje kwako?Sijui ila ninachokumbuka ni kwamba gwiji la muziki nchini Tanzania,Hayati Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba kwamba Mapenzi Hayana Dawa.Msikilize Sagna kisha useme yaliyoko moyoni mwako.

Read more:- BongoCelebrity

No comments:

Post a Comment