amreezle

amreezle

Thursday, October 20, 2011

Habari mbalimbali ambazo zinazidi kusambaa mtandaoni na pia katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vile vya kimataifa kama vile CNN,zinasema kwamba aliyekuwa Rais wa Libya,Moammar Ghadhafi amefariki dunia baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya katika mapambano makali yaliyotokea katika mji aliozaliwa wa Sirte kati ya waasi(National Transitional Council-NTC) na majeshi yake.Kwa mujibu wa msemaji wa NTC,Abdel Majid Mlegta,Ghadhafi amefariki kutokana na kuumizwa vibaya kichwani wakati wa mashambulizi hayo.
Hizi hapa ni baadhi ya picha ambazo zinazidi kusambaa mtandaoni zinazoonyesha sura ya Moammar Ghadhafi baada ya mashambulizi.Tunaomba radhi kwa picha hizi!
Ghadhafi?
Bado tunaendelea kufuatilia kwa makini habari hizi kwani bado hazijathibitishwa rasmi.Stay tuned

Read more: afrotanza.blog

No comments:

Post a Comment