WOLPER: IGENI NA STAILI HII…
MUUZA nyago classic ndani ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper juzikati alibambwa akiwa na muonekano mpya a.k.a kipara na akionyesha hali ya kujishebedua kwakudai kuwa kama kuna mwenye uwezo jaribu kumuiga kama ataweza kukaa na hali hii.Ishu hiyo ilisanuka pande za Mwenge juzikati baada ya kugongana uso kwa uso na paparazi wa Mateja20 na kummwagia picha hizi ‘current’ zinazomuonesha akiwa katika muonekano wake mpya uliyotokana na kunyoa nywele zake na kubakiza chache alizopaka kitu cha Bleach.
“Hii ni staili yangu nitakayoitumia katika life yangu ya sasa tuone kama wataweza kuiga maana nawajua wabongo wengi walivyo wakishaona tu mtu kafanya jambo likakubalika basi nawao wanaanza kuiga,” alisema Wolper.Hata hivyo kuna baadhi ya wadau ambao wamlimuona na staili hiyo na kutonya kwamba staili hiyo anayojigambia kumbe naye ameiga kutoka kwa staa wa picha za utupu na mwanamuziki kutoka pande za Marekani Amber Rose, na mimi nilipoangalia nikagundua kwa hiyo imefanana na haina ubishi.
Je, kwenu nyie wasomaji wa Mateja20, mnasemaje kuhusiana na hili maana nalazimika kuwashilikisha kutokana nayeye kuanza kuichimbia biti staili hii kwa wengine wasije kumuiga.
Toa maoni yoko hapo chini halafu tuyafanyie kazi ili naye aweze kujua mnasema kwa hilo, maana mimi naamini hapa duniani hakuna kitu cha mtu mmoja.
Labda kama si kushabiana na mwanamuziki kutoka kiwanja, Amber Rose ingawa mwenyewe hajafunguka chochote kuhusu kuiga swagger hizi na kupitia maoni yenu tutamtafuta Wolper afunguke alau kiduchu
No comments:
Post a Comment