amreezle

amreezle

Saturday, October 8, 2011


Wakati muziki ambao leo tunauita wa kizazi kipya unaanza kushika kasi,vijana wengi waliojishughulisha na muziki huo walikuwa wakifokafoka(rap) huku wachache sana wakiimba.Exception ilikuwa kundi la Mawingu…lile la kina Othman Njaidi,Sindila na wenzake.Wengi bado tunawakumbuka na kina Oya Msela…
Miaka michache baadae ukaja wakati ambao wengine wanapenda kuuita mwanzo mpya wa muziki wa kizazi kipya.Hapa ndipo pale watu wazima(wazazi) walipoanza kutega masikio au kusikiliza kwa kina kinachozungumzwa na vijana kupitia muziki wao.Mwanzo huo mpya ndio ulikuwa na nyimbo kama Chemsha Bongo kutoka kundi la Hard Blasterz ndani yake akiwemo Professor Jay(enzi hizo aliitwa Nigga Jay).Wazazi walipokubali,mwamko ulipozidi wakatokea vijana wengine ambao wao wakasema sisi hatutofoka foka.Badala yake tutaimba.Miongoni mwao ndio wanamuziki kama vile Mad Ice(nasikia huyu jamaa alitokea Uganda au wazazi wake ni waganda-sina stori kamili).Kama utakumbuka akatamba sana na wimbo wake Baby Girl. Mitaani vijana wakalipuka…Baby Girl ikawa kawimbo ka taifa fulani.
Baada ya miaka kadhaa,Mad Ice akatimka nchini kwenda zake majuu(Finland) kutafuta majani ya kijani zaidi(green pastures).Huko akaendeleza muziki lakini sio kufyatua album iliyotisha au mambo kama hayo.Pamoja na hayo akawa anazidi kujizolea mashabiki kwa sababu ya kupiga muziki wake live.Wazungu wanapenda zaidi muziki wa live kuliko playback.
Hivi karibuni aliachia single yake ya kwanza kutoka katika EP yake ambayo ameipa jina la Maisha.Single ile iliitwa Te Amo.Sasa kutoka katika EP hiyo hiyo,Mad Ice anaachia kitu kinachokwenda kwa jina Mapenzi Sumu .Usikilize hapo chini kisha useme kama unakubaliana na mimi katika kuona maturity ya kimuziki ya Mad Ice.Kazi kwako.

Read more: Bongo Fleva - BongoCelebrity

No comments:

Post a Comment