AFRIKA KUSINI....WAKATA CONDOMS ZA KICHINA....!
Mahakama ya Pretoria nchini Afrika Kusini imeizuia Serikali ya nchi kununua condoms milioni 11 toka China,wakidai kuwa ni ndogo sana kwa size
Wizara ya Fedha ya nchi hiyo ilikua na mkataba na kampuni iitwayo Siqamba Medical,iliyokua na mpango wa kununua condoms aina ya Phoenurse condoms toka China,na akitoa hukumu hiyo Jaji Sulet Potterill alisema condoms hizo ni ndogo sana, ni feki,na hazijathibitishwa na Shirika la Afya Duniani na hatua hiyo imekuja baada Afika Kusini kuwa na maambukizi mengi zaidi kuliko nchi yoyote duniani,kufikia watu 5.38 milioni kati ya watu milioni 50 wana virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa ukimwi.
No comments:
Post a Comment