ROMA NA KALLA JEREMIAH....MOVEMENT YA PAMOJA...!
Concious Hip-Hopper toka TZ,Roma Mkatoliki ameungana na Rapper Kalla Jeremiah na kuanzisha movement inayoitwa 'Mitaa Ina Njaa Na Kiu....We Are Comin 2 Feed U'
KALLA JEREMIAH
Movement hiyo ina lengo la kumfikia kila mtanzania anapopatikana na kuwapa chakula na vinywaji na imeanzia wilayani Geita mkoa wa Mwanza
WASANII KENYA....WATOA VIDEO YA PAMOJA...!
Artist toka Kenya wameungana na kutoa video iitwayo Kilio ikiwa ni Project ya The Kenyans for Kenya iliyozinduliwa kwa ajili ya kuwahamasisha wasamaria wema kuwachangia brothers and sisters waliokumbwa na baa la njaa
Video hiyo released na artiste kama Juliani, Wyre,Nameless,Wahu,Redsan, Ken Wa Maria,JuaCali,Allan Aaron,Ekko Dydah,MOG wameshiriki kwenye project hiyo inayosimamiwa na Safaricom Kenya
ARTIST RABADABA TOKA UG....KUFUNGA NDOA...?!
Artist Rabadaba toka Uganda,baada ya kuwa na msala kwa miezi kadhaa na Baby mama wake Sheila Ferguson na mdada huyo kufunguka kuwa amemsamehe Rabdaba....za Chini ya Carpet zimefunuliwa kuwa kwa sasa huenda vikao vya harusi vikaanza...soon
RABADABA vs SHEILA FERGUSON
Sheila alifunguka kwenye interview kuwa kwa kuwa wamesameheana, haina kwere kama wakifunga ndoa na kwa sasa malavidavi kama yamekolea hivi,coz Rabadaba amechora tatoo ya jina la Sheila kwenye mkono wake wa kulia na Sheila lake kapiga bonge la tatoo ya jina la ubatizo la Rabadaba,Faisal Sseguya
RAPPER JCB....AACHIA SINGLE MPYA NA HARD MAD...!!
Member toka Kundi la Watengwa la Kijenge ya Juu jijini A-Town,Jacob Makalla aka JCB amedondosha ngoma yake mpya kitaani inakayokwenda kwa jina la Dunia Kizani,akiwa na mkali wa Dancehall TZ,Hard Mad na mkono wa Producer Lamar toka FishCrab ndio umehusika na unyongaji na mishe mishe zote na track hiyo
No comments:
Post a Comment