Mwana FA ft, Linah "YALAITI" Coming sOOn....
Mwana FA msanii mwenye bahati yakutoka kila siku ngoma kali na zinazopendwa na wananchi baada ya kufanya vizuri kwenye video na wimbo wa UNANIJUA UNANISIKI sasa yupo tayari kabisa kuja na wimbo mwingine utakaomshirikisha msanii mdogo Linah kutoka THT.
Juzi wakati tunarudi home nilipata bahati ya kusikilizishwa wimbo huo mpya unaoitwa YALAITI ambao umefanyiwa sample kutoka kwa wasanii wakongwe ambao waliutumia tuka kitambo, hapa namzungumzia Siti, Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude. Wimbo huu kwenye chorus ameimba Linah na kurudia kwa melody ile ile halafu mtu mzima akadondokea. Gitaa limepigwa na mmoja wa walimu wa muziki THT anaitwa Cadinal Gento na biti ameisimamia Marco Chali kutoka MJ Rec
No comments:
Post a Comment