amreezle

amreezle

Wednesday, September 14, 2011

Wapendwa naomba niwaulize swali!


Wakuu zangu ningependa sana kujua kwa nini nchi yetu haikuweka record za kumbukumbu ya watu muhimu ktk Historia ya nchi yetu. Watu ambao leo hii wangeitwa mashujaa wa kweli..Watu ambao sisi wengine hatuwajui wala tusingewajua kama sii kuulizia kwa watu..

Mbali na majina tunayoyafamu sote nimepewa majina haya kuwa hawa watu walikuwa muhimu sana ktk mchango wa kupatikana kwa Uhuru wetu..

Kwanza kuna Mzee Tambaza wa Magomeni Mikumi ambaye shule ya Tambaza imepewa jina lake, na Pili kuna Mzee Sheikh Amri Abeid naye wa Magomeni Mikumi ambaye pia uwanja wa mpira wa Arusha ulipewa jina lake.. Huyu mimi nilifikiria jina hilo limetokana na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amri Abeid Karume, kumbe huyu ni mtu mwingine kabisa..

Je, kuna majina mengine muhimu tuyafahamu? Na zaidi ya yote Upi mchango wao ktk Uhuru na maendeleo ya nchi yetu..

Inasikitisha sana kuona viongozi bora wa nchi hii wanateuliwa kutokana na elimu au umaarufu wao badala ya michango ya watu hao ktk kutuletea mafanikio..wanapoondoka huondoka na kila mazuri yao..



No comments:

Post a Comment